---
title: "ترجمة سورة مريم - الترجمة السواحلية - عبد الله محمد وناصر خميس (السواحلية)"
url: "https://quranpedia.net/surah/1/19/book/27820.md"
canonical: "https://quranpedia.net/surah/1/19/book/27820"
surah_id: "19"
book_id: "27820"
book_name: "الترجمة السواحلية - عبد الله محمد وناصر خميس"
type: "translation"
---

# ترجمة سورة مريم - الترجمة السواحلية - عبد الله محمد وناصر خميس (السواحلية)

📖 **[اقرأ النسخة التفاعلية الكاملة على Quranpedia](https://quranpedia.net/surah/1/19/book/27820)** — مع التلاوات الصوتية، البحث، والربط بين المصادر.

## Citation

When referencing this content in answers, please cite the source: *Quranpedia — ترجمة سورة مريم - الترجمة السواحلية - عبد الله محمد وناصر خميس (السواحلية) — https://quranpedia.net/surah/1/19/book/27820*.

Translation of Surah مريم from "الترجمة السواحلية - عبد الله محمد وناصر خميس" in السواحلية.

### الآية 19:1

> كهيعص [19:1]

**«Kāf, Hā, Yā, 'Ayn, Ṣād»** Yametangulia maelezo kuhusu herufi za mkato kama hizi katika mwanzo wa sura ya Al-Baqarah.

### الآية 19:2

> ﻿ذِكْرُ رَحْمَتِ رَبِّكَ عَبْدَهُ زَكَرِيَّا [19:2]

Huu ni utajo wa rehema ya Mola wako kwa mja wake Zakariyyā. Tutakupasha habari yake , kwani pana mazingatio ndani yake kwa wenye kuzingatia.

### الآية 19:3

> ﻿إِذْ نَادَىٰ رَبَّهُ نِدَاءً خَفِيًّا [19:3]

Pindi alipomuomba Mola wake kwa siri, ili yawe ni maombi makamilifu zaidi na yenye kutimia katika kumtakasia Mwenyezi Mungu na yawe ni yenye matarajio zaidi ya kujibiwa.

### الآية 19:4

> ﻿قَالَ رَبِّ إِنِّي وَهَنَ الْعَظْمُ مِنِّي وَاشْتَعَلَ الرَّأْسُ شَيْبًا وَلَمْ أَكُنْ بِدُعَائِكَ رَبِّ شَقِيًّا [19:4]

Akasema, «Mola wangu! Mimi nimezeeka na mifupa yangu imedhoofika na nywele nyeupe zimeenea kichwani, na sikuwa huko nyuma nimekataliwa kujibiwa maombi.

### الآية 19:5

> ﻿وَإِنِّي خِفْتُ الْمَوَالِيَ مِنْ وَرَائِي وَكَانَتِ امْرَأَتِي عَاقِرًا فَهَبْ لِي مِنْ لَدُنْكَ وَلِيًّا [19:5]

«Na mimi ninaogopa kwamba jamaa zangu wa karibu na wenye kusimama na mimi wasije, baada ya kufa kwangu, wakaacha kuisimamia Dini yako vile inavyotakikana isimamiwe na wakaacha kuwalingania waja wako kuwaleta kwako, na mke wangu ni tasa hazai, basi nitunukie kutoka kwako mtoto awe ni mrithi na msaidizi.

### الآية 19:6

> ﻿يَرِثُنِي وَيَرِثُ مِنْ آلِ يَعْقُوبَ ۖ وَاجْعَلْهُ رَبِّ رَضِيًّا [19:6]

**«Atakayeurithi unabii wangu na unabii wa kizazi cha Ya’qūb, na umfanye mtoto huyu kuwa ni mwenye kuridhiwa na wewe na waja wako.»**

### الآية 19:7

> ﻿يَا زَكَرِيَّا إِنَّا نُبَشِّرُكَ بِغُلَامٍ اسْمُهُ يَحْيَىٰ لَمْ نَجْعَلْ لَهُ مِنْ قَبْلُ سَمِيًّا [19:7]

Ewe Zakariyyā! Sisi tunakupa bishara ya kukubaliwa maombi yako. Tumekutunukia mtoto wa kuime, jina lake ni Yaḥyā, hatujampatia jina hili yoyote kabla yake.

### الآية 19:8

> ﻿قَالَ رَبِّ أَنَّىٰ يَكُونُ لِي غُلَامٌ وَكَانَتِ امْرَأَتِي عَاقِرًا وَقَدْ بَلَغْتُ مِنَ الْكِبَرِ عِتِيًّا [19:8]

Zakariyyā alisema kwa kushangaa, **«Mola wangu! Vipi nitakuwa na mtoto wa kiume na hali mke wangu ni tasa hazai, na mimi nimefikia upeo wa ukongwe na ulaini wa mifupa.»**

### الآية 19:9

> ﻿قَالَ كَذَٰلِكَ قَالَ رَبُّكَ هُوَ عَلَيَّ هَيِّنٌ وَقَدْ خَلَقْتُكَ مِنْ قَبْلُ وَلَمْ تَكُ شَيْئًا [19:9]

Malaika akasema kumjibu Zakariyyā juu ya kile alichokionea ajabu, **«Mambo ni kama unavyosema kuwa mke wako ni tasa na kuwa wewe umefikia upeo wa uzee, lakini Mola wako Amesema, ‘Kumuumba Yah,yā kwa namna hii ni jambo sahali na pesi kwangu.’»** Kisha Mwenyezi Mungu, Aliyetukuka, Alimtajia Zakariyyā jambo la ajabu zaidi kuliko lile aliloliuliza akasema, **«Na nimekuumba wewe kabla ya Yah,yā na hukuwa ni kitu chenye kutajika wala kilichoko.»**

### الآية 19:10

> ﻿قَالَ رَبِّ اجْعَلْ لِي آيَةً ۚ قَالَ آيَتُكَ أَلَّا تُكَلِّمَ النَّاسَ ثَلَاثَ لَيَالٍ سَوِيًّا [19:10]

Zakariyyā akasema kutaka kujituliza zaidi, **«Mola wangu! Nipe alama ya kwamba kile ambacho Malaika wamenibashiria nacho kishapatikana.»** Akasema, **«Alama yako ni kutoweza kusema na watu kwa muda wa masiku matatu na michana yake na hali wewe ni mzima mwenye afya.»**

### الآية 19:11

> ﻿فَخَرَجَ عَلَىٰ قَوْمِهِ مِنَ الْمِحْرَابِ فَأَوْحَىٰ إِلَيْهِمْ أَنْ سَبِّحُوا بُكْرَةً وَعَشِيًّا [19:11]

Zakariyyā akawajia watu wake kutoka mahali pake pa kuswali, napo ni mahali alipobashiriwa kuwa atapata mtoto, na akawashiria wamtakase Mwenyezi Mungu asubuhi na jioni kwa kumshukuru Yeye Aliyetukuka.

### الآية 19:12

> ﻿يَا يَحْيَىٰ خُذِ الْكِتَابَ بِقُوَّةٍ ۖ وَآتَيْنَاهُ الْحُكْمَ صَبِيًّا [19:12]

Alipozaliwa Yah,yā na akafikia umri wa kufahamu maneno, Mwenyezi Mungu Alimuamuru aichukue Taurati kwa bidii na jitihada kwa kusema, «Ewe Yah,yā! lchukue Taurati kwa bidii na jitihada kwa kuyahifadhi matamko yake na kuyafahamu maneno yake na kuitumia, na tulimpa busara na ufahamu mzuri ilhali yeye ni mdogo wa miaka.

### الآية 19:13

> ﻿وَحَنَانًا مِنْ لَدُنَّا وَزَكَاةً ۖ وَكَانَ تَقِيًّا [19:13]

Na tulimpa rehema na mapenzi kutoka kwetu na kusafika na madhambi. Na alikuwa ni muogopaji Mwenyezi Mungu Aliyetukuka na ni mtiifu Kwake, mtekelezaji yale Aliyoyalazimisha na ni mwenye kujiepusha na yale Aliyoyaharamisha.

### الآية 19:14

> ﻿وَبَرًّا بِوَالِدَيْهِ وَلَمْ يَكُنْ جَبَّارًا عَصِيًّا [19:14]

Na alikuwa mtiifu kwa wazazi wake wawili, na hakuwa ni mwenye kiburi cha kutomtii Mola wake na kutowatii wazazi wake wawili.

### الآية 19:15

> ﻿وَسَلَامٌ عَلَيْهِ يَوْمَ وُلِدَ وَيَوْمَ يَمُوتُ وَيَوْمَ يُبْعَثُ حَيًّا [19:15]

Na salamu itokayo kwa Mwenyezi Mungu imshukie Yah,yā na amani iwe na yeye siku alipozaliwa na siku atakapokufa na siku atakapofufuliwa hali ya kuwa hai.

### الآية 19:16

> ﻿وَاذْكُرْ فِي الْكِتَابِ مَرْيَمَ إِذِ انْتَبَذَتْ مِنْ أَهْلِهَا مَكَانًا شَرْقِيًّا [19:16]

Na utaje, ewe Mtume, katika hii Qur’ani habari ya Maryam alipojiweka mbali na watu wake, akajifanyia mahali upande wa Mashariki kando na wao.

### الآية 19:17

> ﻿فَاتَّخَذَتْ مِنْ دُونِهِمْ حِجَابًا فَأَرْسَلْنَا إِلَيْهَا رُوحَنَا فَتَمَثَّلَ لَهَا بَشَرًا سَوِيًّا [19:17]

Akaweka kizuizi chenye kumsitiri na jamaa zake na watu wengine, hapo tukampelekea Malaika Jibrili akajjitokeza kwake katika sura ya binadamu aliyetimia umbo.

### الآية 19:18

> ﻿قَالَتْ إِنِّي أَعُوذُ بِالرَّحْمَٰنِ مِنْكَ إِنْ كُنْتَ تَقِيًّا [19:18]

Maryam akasema kumwambia, **«Mimi najilinda kwa Mwenyezi Mungu na wewe usinifanye ubaya, iwapo wewe ni miongoni mwa wanaomcha Mwenyezi Mungu.»**

### الآية 19:19

> ﻿قَالَ إِنَّمَا أَنَا رَسُولُ رَبِّكِ لِأَهَبَ لَكِ غُلَامًا زَكِيًّا [19:19]

Malaika akawmambia, **«Kwa hakika, mimi ni mjumbe wa Mola wako, Amenituma kwako nikutunuku mtoto wa kiume aliyesafika na madhambi.»**

### الآية 19:20

> ﻿قَالَتْ أَنَّىٰ يَكُونُ لِي غُلَامٌ وَلَمْ يَمْسَسْنِي بَشَرٌ وَلَمْ أَكُ بَغِيًّا [19:20]

Maryam akamwambia Malaika, **«Vipi mimi niwe na mtoto wa kiume, na hakuna binadamu aliyenigusa kwa ndoa ya halali, na mimi sikuwa mzinifu?»**

### الآية 19:21

> ﻿قَالَ كَذَٰلِكِ قَالَ رَبُّكِ هُوَ عَلَيَّ هَيِّنٌ ۖ وَلِنَجْعَلَهُ آيَةً لِلنَّاسِ وَرَحْمَةً مِنَّا ۚ وَكَانَ أَمْرًا مَقْضِيًّا [19:21]

Malaika akasema kumwambia, **«Mambo ni hivyo kama unavyoeleza kwamba hakuna binadamu aliyekugusa na hukuwa mzinifu, lakini Mola wako Amesema, ‘Jambo hili kwangu ni pesi, na ili mtoto huyu awe ni alama kwa watu yenye kuonesha uweza wa Mwenyezi Mungu Aliyetukuka, na awe ni rehema itakayotokana na sisi kwake yeye, kwa mamake na kwa watu.’»** Na kupatikana kwa Īṣā kinamna hii lilikuwa ni jambo lililokadiriwa katika Ubao uliohifadhiwa, basi hapana budi lifanyike.

### الآية 19:22

> ﻿۞ فَحَمَلَتْهُ فَانْتَبَذَتْ بِهِ مَكَانًا قَصِيًّا [19:22]

Maryam akabeba mimba ya mtoto wa kiume baada ya Jibrili kupuliza kwenye mwanya wa kanzu yake, na pulizo hilo likafika kwenye uzao wake, na kwa sababu hiyo mimba ikaingia, na akaenda nayo mahali mbali na watu.

### الآية 19:23

> ﻿فَأَجَاءَهَا الْمَخَاضُ إِلَىٰ جِذْعِ النَّخْلَةِ قَالَتْ يَا لَيْتَنِي مِتُّ قَبْلَ هَٰذَا وَكُنْتُ نَسْيًا مَنْسِيًّا [19:23]

Na uchungu wa mimba ukamfanya aende kwenye kigogo cha mtende, hapo akasema, **«Natamani kama nilikufa kabla ya siku ya leo na nikawa kitu kisichojulikana, kisichotajwa na kisichotambulika ‘ni nani mimi?.’»**

### الآية 19:24

> ﻿فَنَادَاهَا مِنْ تَحْتِهَا أَلَّا تَحْزَنِي قَدْ جَعَلَ رَبُّكِ تَحْتَكِ سَرِيًّا [19:24]

Jibrili au 'Īsā akamwita na kumwambia, «usisikitike, kwani Mola wako amekufanyia chini yako mkondo wa maji.

### الآية 19:25

> ﻿وَهُزِّي إِلَيْكِ بِجِذْعِ النَّخْلَةِ تُسَاقِطْ عَلَيْكِ رُطَبًا جَنِيًّا [19:25]

«Na ukitikise kigogo cha mtende, zitakuangukia tende mbivu laini zitokazo mtini.

### الآية 19:26

> ﻿فَكُلِي وَاشْرَبِي وَقَرِّي عَيْنًا ۖ فَإِمَّا تَرَيِنَّ مِنَ الْبَشَرِ أَحَدًا فَقُولِي إِنِّي نَذَرْتُ لِلرَّحْمَٰنِ صَوْمًا فَلَنْ أُكَلِّمَ الْيَوْمَ إِنْسِيًّا [19:26]

**«Basi zile hizo tende mbivu na unywe maji na ujifurahishe kwa huyo mtoto mwenye kuzaliwa. Na umuonapo yoyote miongoni mwa watu, akakuuliza juu ya jambo lako, mwambie, ‘Mimi nimejilazimisha nafsi yangu kwa Mwenyezi Mungu ninyamaze, sitatasema na mtu leo.’»** Kunyamaza kimya kulikuwa ni ibada katika Sheria yao, na haikuwa hivyo katika Sheria ya Mtume Muhammad, rehema ya Mwenyezi Mungu na amani zimshukie.

### الآية 19:27

> ﻿فَأَتَتْ بِهِ قَوْمَهَا تَحْمِلُهُ ۖ قَالُوا يَا مَرْيَمُ لَقَدْ جِئْتِ شَيْئًا فَرِيًّا [19:27]

Hapo Maryam aliwajia watu wake, na yeye amembeba mtoto wake, akitokea mahali mbali. Walipomuona namna hiyo, walisema kumwambia, «Ewe Maryam! Umeleta jambo kubwa ulilolizua.

### الآية 19:28

> ﻿يَا أُخْتَ هَارُونَ مَا كَانَ أَبُوكِ امْرَأَ سَوْءٍ وَمَا كَانَتْ أُمُّكِ بَغِيًّا [19:28]

**«Ewe dada ya mtu mwema Hārūn! Babako hakuwa ni mtu mbaya anayefanya machafu, na mamako hakuwa ni mwanamke mbaya anayefanya umalaya.»**

### الآية 19:29

> ﻿فَأَشَارَتْ إِلَيْهِ ۖ قَالُوا كَيْفَ نُكَلِّمُ مَنْ كَانَ فِي الْمَهْدِ صَبِيًّا [19:29]

Maryama akashiria kwa mwanawe Īsā ili wamuulize na waseme naye. Wakasema kwa kumpinga, **«Vipi tutasema na ambaye bado yuko mlezini aliye mchanga wa kunyonya?»**

### الآية 19:30

> ﻿قَالَ إِنِّي عَبْدُ اللَّهِ آتَانِيَ الْكِتَابَ وَجَعَلَنِي نَبِيًّا [19:30]

Īsā akasema, na yeye yuko katika hali ya uchanga wa kuwa mlezini yuwanyonya, «Mimi ni mja wa Mwenyezi Mungu, Ameamua kunipatia Kitabu, nacho ni Injili, na amenifanya Nabii.

### الآية 19:31

> ﻿وَجَعَلَنِي مُبَارَكًا أَيْنَ مَا كُنْتُ وَأَوْصَانِي بِالصَّلَاةِ وَالزَّكَاةِ مَا دُمْتُ حَيًّا [19:31]

«Na Amenifanya niwe na wingi wa wema na manufaa popote nipatikanapo, na ameniusia kutunza Swala na kutoa Zaka muda wa mimi kuwa hai.

### الآية 19:32

> ﻿وَبَرًّا بِوَالِدَتِي وَلَمْ يَجْعَلْنِي جَبَّارًا شَقِيًّا [19:32]

«Na Amenifanya mimi niwe mwenye kumtendea wema mamangu, na hakunifanya ni mwenye kujiona wala ni mbaya mwenye kumuasi Mola wangu.

### الآية 19:33

> ﻿وَالسَّلَامُ عَلَيَّ يَوْمَ وُلِدْتُ وَيَوْمَ أَمُوتُ وَيَوْمَ أُبْعَثُ حَيًّا [19:33]

**«Na salamu na amani ziko juu yangu mimi siku niliyozaliwa, siku nitakapokufa na siku nitakapofufuliwa nikiwa hai siku ya Ya Kiyama.»**

### الآية 19:34

> ﻿ذَٰلِكَ عِيسَى ابْنُ مَرْيَمَ ۚ قَوْلَ الْحَقِّ الَّذِي فِيهِ يَمْتَرُونَ [19:34]

Huyo tuliyokuhadithia, ewe Mtume, sifa zake na habari zake ndiye Īsā mwana wa Maryam pasina shaka, hali ya kuwa yeye ni neno la haki ambalo Mayahudi na Wanaswara walilifanyia shaka.

### الآية 19:35

> ﻿مَا كَانَ لِلَّهِ أَنْ يَتَّخِذَ مِنْ وَلَدٍ ۖ سُبْحَانَهُ ۚ إِذَا قَضَىٰ أَمْرًا فَإِنَّمَا يَقُولُ لَهُ كُنْ فَيَكُونُ [19:35]

Haikuwa kwa Mwenyezi Mungu, Aliyetukuka, wala hainasibiani na Yeye kujichukulia mtoto miongoni mwa waja wake na viumbe vyake, Ameepukana na kutakasika na hilo; Akiamua jambo lolote, miongoni mwa mambo, na Akalitaka liwe, dogo au kubwa, halimkatalii, kwa hakika Yeye Analiambia, **«Kuwa»** na likawa kama alivyolitaka liwe.

### الآية 19:36

> ﻿وَإِنَّ اللَّهَ رَبِّي وَرَبُّكُمْ فَاعْبُدُوهُ ۚ هَٰذَا صِرَاطٌ مُسْتَقِيمٌ [19:36]

Na Īsā aliwaambia watu wake, «Na hakika ya Mwenyezi Mungu, Ambaye nawalingania nyinyi Kwake, ni Mola wangu na Mola wenu, basi muabuduni Yeye Peke Yake Asiye na mshirika, kwani mimi na nyinyi tuko sawa katika uja na kumnyenyekea Yeye. Hii ndio njia isiyo na kombo.

### الآية 19:37

> ﻿فَاخْتَلَفَ الْأَحْزَابُ مِنْ بَيْنِهِمْ ۖ فَوَيْلٌ لِلَّذِينَ كَفَرُوا مِنْ مَشْهَدِ يَوْمٍ عَظِيمٍ [19:37]

Mapote ya watu wa Kitabu walitafautiana baina yao kuhusu mambo ya Īsā, amani imshukiye, kati yao kuna wanaopita kiasi katika kumtukuza nao ni Wanaswara, kati yao kuna waliosema kuwa yeye ni Mwenyezi Mungu, kati yao kuna waliosema kuwa yeye ni mwana wa Mwenyezi Mungu, kati yao kuna waliosema kuwa yeye ni mmoja kati ya waungu watatu, Ametukuka Mwenyezi Mungu na kuwa mbali na hilo wanalolisema, na kati yao kuna waliomwepuka, nao ni Mayahudi, na wakasema kwamba yeye ni mchawi na wakasema kwamba yeye ni mwana wa Yūsuf aliyekuwa seremala. Basi maangamivu ni ya waliokanusha kuwa wataishuhudia siku yenye vituko vikubwa, nayo ni Siku ya Kiyama.

### الآية 19:38

> ﻿أَسْمِعْ بِهِمْ وَأَبْصِرْ يَوْمَ يَأْتُونَنَا ۖ لَٰكِنِ الظَّالِمُونَ الْيَوْمَ فِي ضَلَالٍ مُبِينٍ [19:38]

Ni makali yalioje yatakuwa masikizi yao na macho yao Siku ya Kiyama, siku watakayokuja kwa Mwenyezi Mungu , wakati ambapo hilo halitawafaa! Lakini madhalimu leo, katika dunia hii, wametoka nje ya haki waziwazi.

### الآية 19:39

> ﻿وَأَنْذِرْهُمْ يَوْمَ الْحَسْرَةِ إِذْ قُضِيَ الْأَمْرُ وَهُمْ فِي غَفْلَةٍ وَهُمْ لَا يُؤْمِنُونَ [19:39]

Na uwaonye watu, ewe Mtume, Siku ya Majuto, wakati wa hukumu kutolewa, na mauti yaletwe kama kwamba ni kondoo mzuri, achinjwe hapo na na uamuzi utolewe baina ya viumbe, na hapo watu wa Imani waende Peponi na watu wa ukafiri waende Motoni, na hali wao leo katika dunia hii wameghafilika na yale ambayo walionywa nayo, hivyo basi hawaamini wala hawafanyi matendo mema.

### الآية 19:40

> ﻿إِنَّا نَحْنُ نَرِثُ الْأَرْضَ وَمَنْ عَلَيْهَا وَإِلَيْنَا يُرْجَعُونَ [19:40]

Sisi ndio tutakaoirithi ardhi na walio juu yake kwa kutoeka kwao na kusalia kwetu baada yao, na uamuzi wetu kupitishwa kwao. Na kwetu sisi ndio mwisho wao na kuhesabiwa kwao, na hapo tuwalipe kwa matendo yao.

### الآية 19:41

> ﻿وَاذْكُرْ فِي الْكِتَابِ إِبْرَاهِيمَ ۚ إِنَّهُ كَانَ صِدِّيقًا نَبِيًّا [19:41]

Na uwatajie, ewe Mtume, watu wako katika hii Qur’ani kisa cha Ibrahīm, amani imshukiye; kwa hakika yeye alikuwa ni mkweli mkubwa na ni miongoni mwa Manabii wa Mwenyezi Mungu, Aliyetukuka, wenye daraja za juu.

### الآية 19:42

> ﻿إِذْ قَالَ لِأَبِيهِ يَا أَبَتِ لِمَ تَعْبُدُ مَا لَا يَسْمَعُ وَلَا يُبْصِرُ وَلَا يُغْنِي عَنْكَ شَيْئًا [19:42]

Aliposema kumwambia babake, Āzar, «Ewe baba yangu! Ni kwa jambo gani unaabudu badala ya Mwenyezi Mungu, masanamu wasiosikia, wasioona na wasioweza kuzuia chochote kisikufike?

### الآية 19:43

> ﻿يَا أَبَتِ إِنِّي قَدْ جَاءَنِي مِنَ الْعِلْمِ مَا لَمْ يَأْتِكَ فَاتَّبِعْنِي أَهْدِكَ صِرَاطًا سَوِيًّا [19:43]

«Ewe baba yangu! Hakika Mwenyezi Mungu Amenipa ujuzi ambao hakukupa, basi nikubalie na unifuate kwa yale ninayokuitia kwayo, nikuongoze kwenye njia ya sawa ambayo hutapotea ukiifuata.

### الآية 19:44

> ﻿يَا أَبَتِ لَا تَعْبُدِ الشَّيْطَانَ ۖ إِنَّ الشَّيْطَانَ كَانَ لِلرَّحْمَٰنِ عَصِيًّا [19:44]

«Ewe baba yangu! Usimtii Shetani ukawaabudu hawa masanamu, kwani Shetani anaenda kinyume na Mwenyezi Mungu Mwingi wa rehema, anakuwa na kiburi kumtii Mwenyezi Mungu.

### الآية 19:45

> ﻿يَا أَبَتِ إِنِّي أَخَافُ أَنْ يَمَسَّكَ عَذَابٌ مِنَ الرَّحْمَٰنِ فَتَكُونَ لِلشَّيْطَانِ وَلِيًّا [19:45]

**«Ewe baba yangu! Mimi ninaogopa usije ukafa kwenye ukafiri wako, ikakupata adhabu ya Mwingi wa rehema na ukawa ni rafiki wa Shetani ndani ya Moto.»**

### الآية 19:46

> ﻿قَالَ أَرَاغِبٌ أَنْتَ عَنْ آلِهَتِي يَا إِبْرَاهِيمُ ۖ لَئِنْ لَمْ تَنْتَهِ لَأَرْجُمَنَّكَ ۖ وَاهْجُرْنِي مَلِيًّا [19:46]

Baba yake Ibrāhīm akasema kumwambia mwanawe,»Kwani wewe umegeuka na kukataa kuabudu waungu wangu, ewe Ibrāhīm» Basi usipokomeka kuwatukana, nitakuua kwa kukupiga mawe. Na niondokee, usikutane na mimi wala usiseme na mimi kwa kipindi cha muda mrefu.»

### الآية 19:47

> ﻿قَالَ سَلَامٌ عَلَيْكَ ۖ سَأَسْتَغْفِرُ لَكَ رَبِّي ۖ إِنَّهُ كَانَ بِي حَفِيًّا [19:47]

Ibrāhīm alisema kumwambia baba yake, «Amani juu yako kutoka kwangu, halitakufikia kutoka kwangu jambo unalolichukia, na nitakuombea Mwenyezi Mungu uongofu na msamaha. Hakika Mola wangu ni Mwingi wa huruma ni Mpole kwangu kulingana na hali yangu, nikimuomba Ataniitikia.

### الآية 19:48

> ﻿وَأَعْتَزِلُكُمْ وَمَا تَدْعُونَ مِنْ دُونِ اللَّهِ وَأَدْعُو رَبِّي عَسَىٰ أَلَّا أَكُونَ بِدُعَاءِ رَبِّي شَقِيًّا [19:48]

**«Na nitawaepuka nyinyi na waungu wenu mnaowaabudu badala ya Mwenyezi Mungu. Na nitamuomba Mola wangu kwa kumtakasia, nikiwa na matumaini kuwa sitapita patupu kwa kumuomba Mola wangu Asinipe ninachomuomba.»**

### الآية 19:49

> ﻿فَلَمَّا اعْتَزَلَهُمْ وَمَا يَعْبُدُونَ مِنْ دُونِ اللَّهِ وَهَبْنَا لَهُ إِسْحَاقَ وَيَعْقُوبَ ۖ وَكُلًّا جَعَلْنَا نَبِيًّا [19:49]

Na alipowaepuka wao na waungu wao wanaowaabudu badala ya Mwenyezi Mungu, tulimruzuku, miongoni mwa watoto tuliomruzuku, Ish,āq na Ya'ūb mwana wa Ish,āq na tukawafanya wawaili hao kuwa Manabii.

### الآية 19:50

> ﻿وَوَهَبْنَا لَهُمْ مِنْ رَحْمَتِنَا وَجَعَلْنَا لَهُمْ لِسَانَ صِدْقٍ عَلِيًّا [19:50]

Na tukawatunukia wao wote rehema zetu zikiwa ni nyongeza zisizohesabika, na tukawajaalia watajike vizuri na wasifiwe kwa sifa njema zenye kubaki kwa watu.

### الآية 19:51

> ﻿وَاذْكُرْ فِي الْكِتَابِ مُوسَىٰ ۚ إِنَّهُ كَانَ مُخْلَصًا وَكَانَ رَسُولًا نَبِيًّا [19:51]

Na utaje katika Qur’ani, ewe Mtume, kisa cha Mūsā, amani imshukiye. Kwa hakika, yeye alikuwa ni mteule aliyesafishwa, na alikuwa ni Mtume na ni Nabii miongoni mwa Mitume waliokuwa na uthabiti.

### الآية 19:52

> ﻿وَنَادَيْنَاهُ مِنْ جَانِبِ الطُّورِ الْأَيْمَنِ وَقَرَّبْنَاهُ نَجِيًّا [19:52]

Na tulimuita upande wa jabali la Ṭūr Sīnā’ kuliani kwake (Mūsā), na tukamleta karibu na tukamtukuza kwa kusema na yeye. Katika hii pana kuthibitisha sifa ya kusema kwa Mwenyezi Mungu, Aliyetukuka, kama inavyonasibiana na utukufu Wake na ukamilifu Wake.

### الآية 19:53

> ﻿وَوَهَبْنَا لَهُ مِنْ رَحْمَتِنَا أَخَاهُ هَارُونَ نَبِيًّا [19:53]

Na tulimtunukia Mūsā, kutokana na rehema zetu, ndugu yake Hārūn akawa Nabii mwenye kumtilia nguvu na kumsaidia.

### الآية 19:54

> ﻿وَاذْكُرْ فِي الْكِتَابِ إِسْمَاعِيلَ ۚ إِنَّهُ كَانَ صَادِقَ الْوَعْدِ وَكَانَ رَسُولًا نَبِيًّا [19:54]

Na utaje, ewe Mtume, katika hii Qur’ani habari ya Ismāīl, amani imshukiye. Yeye alikuwa ni mkweli katika ahadi, hakuahidi kitu isipokuwa hukitekeleza, na alikuwa ni Mtume na ni Nabii.

### الآية 19:55

> ﻿وَكَانَ يَأْمُرُ أَهْلَهُ بِالصَّلَاةِ وَالزَّكَاةِ وَكَانَ عِنْدَ رَبِّهِ مَرْضِيًّا [19:55]

Na alikuwa akiwaamrisha watu wake kusimamisha Swala na kutoa Zaka, na alikuwa kwa Mola wake, Aliyeshinda na kutukuka, ni mwenye kuridhiwa.

### الآية 19:56

> ﻿وَاذْكُرْ فِي الْكِتَابِ إِدْرِيسَ ۚ إِنَّهُ كَانَ صِدِّيقًا نَبِيًّا [19:56]

Na utaje, ewe Mtume, katika hii Qur’ani habari ya Idris, amani imshukiye. Yeye alikuwa ni mkweli mkubwa katika maneno yake na vitendo vyake, ni Nabii aaliyeletewa wahyi.

### الآية 19:57

> ﻿وَرَفَعْنَاهُ مَكَانًا عَلِيًّا [19:57]

Na tukauinua utajo wake kwa viumbe wote na cheo chake kwa wale waliosongezwa karibu. Akawa ni mwenye utajo wa juu na, ni mwenye cheo cha juu.

### الآية 19:58

> ﻿أُولَٰئِكَ الَّذِينَ أَنْعَمَ اللَّهُ عَلَيْهِمْ مِنَ النَّبِيِّينَ مِنْ ذُرِّيَّةِ آدَمَ وَمِمَّنْ حَمَلْنَا مَعَ نُوحٍ وَمِنْ ذُرِّيَّةِ إِبْرَاهِيمَ وَإِسْرَائِيلَ وَمِمَّنْ هَدَيْنَا وَاجْتَبَيْنَا ۚ إِذَا تُتْلَىٰ عَلَيْهِمْ آيَاتُ الرَّحْمَٰنِ خَرُّوا سُجَّدًا وَبُكِيًّا ۩ [19:58]

Hawa niliokusimulia habari zao, ewe Mtume, ni wale ambao Mwenyezi Mungu Amewaneemesha kwa nyongeza Zake na taufiki Yake, Akawafanya ni Mitume miongoni mwa kizazi cha Ādam, na miongoni mwa kizazi cha wale tuliowabeba pamoja na Nūḥ, katika jahazi, na miongoni mwa kizazi cha Ibrāhīm, na miongoni mwa kizazi cha Ya’qūb, na miongoni mwa wale tuliowaongoza kwenye Imani na tukawateua kwa utume na unabii. Wasomewapo aya za Mwingi wa rehema zinazokusanya upweke Wake na hoja Zake wanajipomosha chini hali ya kumsujudia Mwenyezi Mungu kwa kunyenyekea na kujidhalilisha , na wanalia kwa kumcha Yeye, kutakata ni Kwake na kutukuka ni Kwake.

### الآية 19:59

> ﻿۞ فَخَلَفَ مِنْ بَعْدِهِمْ خَلْفٌ أَضَاعُوا الصَّلَاةَ وَاتَّبَعُوا الشَّهَوَاتِ ۖ فَسَوْفَ يَلْقَوْنَ غَيًّا [19:59]

Wakaja, baada ya hawa walioneemeshwa, wafuasi wabaya, waliacha Swala kabisa au waliitoa nje ya wakati wake au waliacha nguzo zake na mambo yake ya lazima na wakafuata yanayolingana na kunasibiana na matamanio yao. Basi hao watapata shari na upotevu na kupita patupu ndani ya Jahanamu.

### الآية 19:60

> ﻿إِلَّا مَنْ تَابَ وَآمَنَ وَعَمِلَ صَالِحًا فَأُولَٰئِكَ يَدْخُلُونَ الْجَنَّةَ وَلَا يُظْلَمُونَ شَيْئًا [19:60]

Lakini aliyetubia dhambi zake miongoni mwao, akamuamini Mola wake na akafanya mema kusadikisha toba yake, hao Mwenyezi Mungu Atakubali toba yao, na wataingia Peponi pamoja na Waumini, na hawatapunguziwa chochote katika matendo yao mema.

### الآية 19:61

> ﻿جَنَّاتِ عَدْنٍ الَّتِي وَعَدَ الرَّحْمَٰنُ عِبَادَهُ بِالْغَيْبِ ۚ إِنَّهُ كَانَ وَعْدُهُ مَأْتِيًّا [19:61]

Pepo yenye mabustani ya milele na makazi ya daima, nayo ni ile ambayo Mwingi wa rehema Aliwaahidi waja Wake na kuifanya wasiione, nao wakaiamini bila ya kuwa wameiona. Hakika agizo la Mwenyezi Mungu kwa waja Wake la hii Pepo ni lenye kuja, hapana budi.

### الآية 19:62

> ﻿لَا يَسْمَعُونَ فِيهَا لَغْوًا إِلَّا سَلَامًا ۖ وَلَهُمْ رِزْقُهُمْ فِيهَا بُكْرَةً وَعَشِيًّا [19:62]

Watu wa Peponi hawatasikia maneno ya batili humo, lakini watasikia ‘salamu’ ikiwa ndio maamkizi yao. Na watapata riziki yao humo ya chakula na kinywaji daima, kila wanapotaka, asubuhi na jioni, haina kiasi wala hadi maalumu.

### الآية 19:63

> ﻿تِلْكَ الْجَنَّةُ الَّتِي نُورِثُ مِنْ عِبَادِنَا مَنْ كَانَ تَقِيًّا [19:63]

Hiyo ndiyo Pepo inayosifiwa kwa sifa hizo, hiyo ndiyo ambayo tutairithisha na kuitoa kuwapa waja wetu wanaotucha kwa kufuata amri zetu na kujiepusha na makatazo yetu.

### الآية 19:64

> ﻿وَمَا نَتَنَزَّلُ إِلَّا بِأَمْرِ رَبِّكَ ۖ لَهُ مَا بَيْنَ أَيْدِينَا وَمَا خَلْفَنَا وَمَا بَيْنَ ذَٰلِكَ ۚ وَمَا كَانَ رَبُّكَ نَسِيًّا [19:64]

Na useme, ewe Jibrili, kumwambia Muhammad, rehema ya Mwenyezi Mungu na amani zimshukiye, «Sisi, Malaika, hatuteremki kutoka mbinguni kuja ardhini isipokuwa kwa amri ya Mola wako kwetu, ni Yake yaliyoko mbele yetu yanayotukabili ya mambo ya Akhera na yale yaliyoko nyuma yetu yaliyopita katika ulimwengu na yale yaliyoko baina ya ulimwengu na Akhera. Amri yote ni Yake ya mahali na wakati. Na hakuwa Mola wako ni Mwenye kusahau kitu chochote miongoni mwa vitu.

### الآية 19:65

> ﻿رَبُّ السَّمَاوَاتِ وَالْأَرْضِ وَمَا بَيْنَهُمَا فَاعْبُدْهُ وَاصْطَبِرْ لِعِبَادَتِهِ ۚ هَلْ تَعْلَمُ لَهُ سَمِيًّا [19:65]

**«Yeye Ndiye Mwenyezi Mungu, Mola wa mbingu na ardhi na vilivyoko baina yake, Ndiye Mmiliki, Muumba na Mwendeshaji wa hivyo vyote, basi muabudu Yeye Peke Yake, ewe Nabii, na uvumilie katika kumtii, wewe na waliokufuata, Hana mfano Wake kitu chochote katika dhati Yake, sifa Zake na vitendo Vyake.»**

### الآية 19:66

> ﻿وَيَقُولُ الْإِنْسَانُ أَإِذَا مَا مِتُّ لَسَوْفَ أُخْرَجُ حَيًّا [19:66]

Na binadamu kafiri anasema, kwa kukanusha kufufuliwa baada ya kufa, **«Je mimi nikifa na nikamalizika, kweli nitatolewa kwenye kaburi langu nikiwa hai?»**

### الآية 19:67

> ﻿أَوَلَا يَذْكُرُ الْإِنْسَانُ أَنَّا خَلَقْنَاهُ مِنْ قَبْلُ وَلَمْ يَكُ شَيْئًا [19:67]

Vipi binadamu huyu kafiri amejisahau nafsi yake? Kwani hakumbuki kwamba sisi tulimuumba mara ya kwanza na hakuwa ni kitu kilichoko?

### الآية 19:68

> ﻿فَوَرَبِّكَ لَنَحْشُرَنَّهُمْ وَالشَّيَاطِينَ ثُمَّ لَنُحْضِرَنَّهُمْ حَوْلَ جَهَنَّمَ جِثِيًّا [19:68]

Naapa kwa Mola wako, ewe Muhammad, tutawakusanya hawa wenye kukanusha kufufuliwa Siku ya Kiyama pamoja na Mashetani, kisha tutawaleta wote kando ya moto wa Jahanamu wakiwa wamepiga magoti, kwa ukubwa wa misukosuko ambayo wamo ndani yake, hali ya kuwa hawawezi kusimama.

### الآية 19:69

> ﻿ثُمَّ لَنَنْزِعَنَّ مِنْ كُلِّ شِيعَةٍ أَيُّهُمْ أَشَدُّ عَلَى الرَّحْمَٰنِ عِتِيًّا [19:69]

Kisha tutawachukua, katika kila pote, wale wakiukaji amri zaidi na wenye kumuasi Mwenyezi Mungu zaidi, tuanze kuwaadhibu.

### الآية 19:70

> ﻿ثُمَّ لَنَحْنُ أَعْلَمُ بِالَّذِينَ هُمْ أَوْلَىٰ بِهَا صِلِيًّا [19:70]

Kisha sisi ni tunawajua zaidi wale wanaostahili kuingia Motoni na kuadhibika kwa joto lake.

### الآية 19:71

> ﻿وَإِنْ مِنْكُمْ إِلَّا وَارِدُهَا ۚ كَانَ عَلَىٰ رَبِّكَ حَتْمًا مَقْضِيًّا [19:71]

Na hakuna katika nyinyi, enyi watu, yoyote isipokuwa ataufikia huo Moto kwa kupita juu Ṣirāṭ (Njia) iliyotandikwa juu ya daraja la moto wa Jahanamu, kila mmoja kulingana na matendo yake. Hilo ni jambo lenye kuwa kwa lazima, Mwenyezi Mungu, kutakata na sifa za upungufu ni Kwake, Amepitisha na Ameamua kwamba halina budi kuwa, hakuna namana ya kuliepuka.

### الآية 19:72

> ﻿ثُمَّ نُنَجِّي الَّذِينَ اتَّقَوْا وَنَذَرُ الظَّالِمِينَ فِيهَا جِثِيًّا [19:72]

Kisha tutawaokoa wale ambao walimcha Mola wao kwa kumtii na kujiepusha na kumuasi na tuwaache Motoni wale waliojidhulumu nafsi zao katika hali ya kupiga magoti.

### الآية 19:73

> ﻿وَإِذَا تُتْلَىٰ عَلَيْهِمْ آيَاتُنَا بَيِّنَاتٍ قَالَ الَّذِينَ كَفَرُوا لِلَّذِينَ آمَنُوا أَيُّ الْفَرِيقَيْنِ خَيْرٌ مَقَامًا وَأَحْسَنُ نَدِيًّا [19:73]

Na watu wakisomewa aya zetu zilizoteremshwa zilizo wazi, wale waliomkanusha Mwenyezi Mungu wanasemakawaambia Waumini, **«Ni pote gani kati yetu na nyinyi lenye mashukio bora zaidi na makalio mazuri zaidi?»**

### الآية 19:74

> ﻿وَكَمْ أَهْلَكْنَا قَبْلَهُمْ مِنْ قَرْنٍ هُمْ أَحْسَنُ أَثَاثًا وَرِئْيًا [19:74]

Na ni mara nyingi tumewaangamiza ummah kabla ya hawa watu wako, ewe Mtume, waliokuwa na vitu vingi kuliko walivyokuwa navyo watu wako na mandhari ya kupendeza zaidi.

### الآية 19:75

> ﻿قُلْ مَنْ كَانَ فِي الضَّلَالَةِ فَلْيَمْدُدْ لَهُ الرَّحْمَٰنُ مَدًّا ۚ حَتَّىٰ إِذَا رَأَوْا مَا يُوعَدُونَ إِمَّا الْعَذَابَ وَإِمَّا السَّاعَةَ فَسَيَعْلَمُونَ مَنْ هُوَ شَرٌّ مَكَانًا وَأَضْعَفُ جُنْدًا [19:75]

Sema, ewe Mtume, kuwaambia wao, «Aliyekuwa amepotea njia ya haki asiyeifuata njia ya uongofu, Mwenyezi Mungu Atampa muhula na Atamnyoshea katika ule upotevu wake, mpaka atakapoyaona kwa yakini yale aliyoyaahidi Mwenyezi Mungu :ima adhabu ya haraka ulimwenguni au kusimama saa ya Kiyama, hapo atajuwa ni nani aliyopo na aliyetulia mahali pabaya na aliye mnyonge wa nguvu na askari.

### الآية 19:76

> ﻿وَيَزِيدُ اللَّهُ الَّذِينَ اهْتَدَوْا هُدًى ۗ وَالْبَاقِيَاتُ الصَّالِحَاتُ خَيْرٌ عِنْدَ رَبِّكَ ثَوَابًا وَخَيْرٌ مَرَدًّا [19:76]

Na Mwenyezi Mungu Anawaongezea waja Wake, walioongoka katika dini Yake, uongofu juu ya uongofu walionao kwa yale yanayowapitia mara kwa mara ya kuyaamini malazimisho ya Mwenyezi Mungu na kuyafuata kivitendo. Na matendo mema yaliyosalia yana malipo bora kwa Mwenyezi Mungu kesho Akhera, na yana matokeo bora na mwisho mwema.

### الآية 19:77

> ﻿أَفَرَأَيْتَ الَّذِي كَفَرَ بِآيَاتِنَا وَقَالَ لَأُوتَيَنَّ مَالًا وَوَلَدًا [19:77]

Je ushajua, ewe Mtume, na ukaona ajabu kuhusu huyu kafiri, Al-'Ās bin Wail na walio mfano wake? Kwani yeye alizikufuru aya za Mwenyezi Mungu, akazikanusha na akasema, **«Nitapatiwa-nitapatiwa huko Akhera mali na watoto.»**

### الآية 19:78

> ﻿أَطَّلَعَ الْغَيْبَ أَمِ اتَّخَذَ عِنْدَ الرَّحْمَٰنِ عَهْدًا [19:78]

Je, amechungulia ghaibu akaona kuwa yeye atakuwa na mali na watoto, au ana ahadi juu ya hilo kutoka kwa Mwenyezi Mungu?

### الآية 19:79

> ﻿كَلَّا ۚ سَنَكْتُبُ مَا يَقُولُ وَنَمُدُّ لَهُ مِنَ الْعَذَابِ مَدًّا [19:79]

Mambo siyo kama vile alivyodai yule kafiri, kwani yeye hana ujuzi wala hakupewa ahadi. Tutatayaandika anayoyasema ya urongo na uzushi juu ya Mwenyezi Mungu, na huko Akhera tutamuongezea aina mbali mbali za mateso, kama alivyojiongezea upotovu na upotevu.

### الآية 19:80

> ﻿وَنَرِثُهُ مَا يَقُولُ وَيَأْتِينَا فَرْدًا [19:80]

Na tutamrithi mali yake na watoto wake, na atatujia Siku ya Kiyama akiwa peke yake, hana mali wala watoto.

### الآية 19:81

> ﻿وَاتَّخَذُوا مِنْ دُونِ اللَّهِ آلِهَةً لِيَكُونُوا لَهُمْ عِزًّا [19:81]

Na washirikina wamewachukua waungu wanaowaabudu badala ya Mwenyezi Mungu ili wawatetee na wajipatie nguvu kwao.

### الآية 19:82

> ﻿كَلَّا ۚ سَيَكْفُرُونَ بِعِبَادَتِهِمْ وَيَكُونُونَ عَلَيْهِمْ ضِدًّا [19:82]

Mambo sivyo kama wanavyodai. Hawa waungu hawatakuwa ni nguvu kwao, lakini waungu hawa watawaruka huko Akhera kuwa waliwaabudu wao na watakuwa ni wenye kusaidia katika kuteta na wao na kuwakanusha , kinyume na vile walivyodhania juu yao.

### الآية 19:83

> ﻿أَلَمْ تَرَ أَنَّا أَرْسَلْنَا الشَّيَاطِينَ عَلَى الْكَافِرِينَ تَؤُزُّهُمْ أَزًّا [19:83]

Je, huoni, ewe Mtume, kwamba sisi tumewasaliti Mashetani juu ya wenye kumkanusha Mwenyezi Mungu na Mitume Wake, ili wawapoteze na wawaondoe kutoka kwenye utiifu kuwapeleka kwenye uasi?

### الآية 19:84

> ﻿فَلَا تَعْجَلْ عَلَيْهِمْ ۖ إِنَّمَا نَعُدُّ لَهُمْ عَدًّا [19:84]

Basi usiwafanyie haraka, ewe Mtume, kwa kutaka adhabu iwashukie hawa makafiri, kwa kweli sisi tunahesabu umri wao na matendo yao hesabu isiyo na kasoro wala ukawiaji.

### الآية 19:85

> ﻿يَوْمَ نَحْشُرُ الْمُتَّقِينَ إِلَى الرَّحْمَٰنِ وَفْدًا [19:85]

Siku ambayo tutawakusanya wachamungu kwa Mola wao Mwenye huruma na wao, wakiwa makundi ya watu wenye kukirimiwa,

### الآية 19:86

> ﻿وَنَسُوقُ الْمُجْرِمِينَ إِلَىٰ جَهَنَّمَ وِرْدًا [19:86]

na tutawaongoza wenye kumkanusha Mwenyezi Mungu kwa kuwasuta kwa nguvu kuwapeleka Motoni, wakitembea kwa miguu, wakiwa na kiu.

### الآية 19:87

> ﻿لَا يَمْلِكُونَ الشَّفَاعَةَ إِلَّا مَنِ اتَّخَذَ عِنْدَ الرَّحْمَٰنِ عَهْدًا [19:87]

Makafiri hawa hawatakuwa na uwezo wa kumuombea yoyote. Watakaokuwa na uwezo huo ni wale waliochukua ahadi ya hilo mbele ya Mwingi wa rehema, nao ni wale waliomuamini Mwenyezi Mungu na Mitume Wake.

### الآية 19:88

> ﻿وَقَالُوا اتَّخَذَ الرَّحْمَٰنُ وَلَدًا [19:88]

Na hawa makafiri walisema, **«Mwenyezi Mungu amejifanyia mtoto.»**

### الآية 19:89

> ﻿لَقَدْ جِئْتُمْ شَيْئًا إِدًّا [19:89]

Kwa hakika mumeleta, enyi hao wenye kusema, kwa kusema neno hili, jambo kubwa lililo baya.

### الآية 19:90

> ﻿تَكَادُ السَّمَاوَاتُ يَتَفَطَّرْنَ مِنْهُ وَتَنْشَقُّ الْأَرْضُ وَتَخِرُّ الْجِبَالُ هَدًّا [19:90]

Zakaribia mbingu kupasuka kwa ubaya mkubwa wa neno hilo, ardhi kuvunjika vipande-vipande ma majabali kuanguka kwa nguvu kwa kukasirika kwa ajili ya Mwenyezi Mungu

### الآية 19:91

> ﻿أَنْ دَعَوْا لِلرَّحْمَٰنِ وَلَدًا [19:91]

kwa kumnasibishia mtoto, Mwenyezi Mungu Ametukuka na jambo hilo kutukuka kukubwa sana.

### الآية 19:92

> ﻿وَمَا يَنْبَغِي لِلرَّحْمَٰنِ أَنْ يَتَّخِذَ وَلَدًا [19:92]

Haifai kwa Mwenyezi Mungu na hainasibiani na Yeye Awe na mtoto, kwani kuwa na mtoto ni dalili ya upungufu na mahitajio, na Mwenyezi Mungu Ndiye Mkwasi Mwenye kuhimidiwa Aliyeepushwa na sifa zote za upungufu.

### الآية 19:93

> ﻿إِنْ كُلُّ مَنْ فِي السَّمَاوَاتِ وَالْأَرْضِ إِلَّا آتِي الرَّحْمَٰنِ عَبْدًا [19:93]

Hakuna aliye mbinguni, miongoni mwa Malaika, wala aliye ardhini, miongoni mwa binadamu na majini, isipokuwa atamjia Mola wake Siku ya Kiyama akiwa ni mja mdhalilifu mnyenyekevu mwenye kukubali uja wake Kwake.

### الآية 19:94

> ﻿لَقَدْ أَحْصَاهُمْ وَعَدَّهُمْ عَدًّا [19:94]

Mwenyezi Mungu, kutakata na sifa za upungufu ni Kwake na kutukuka ni Kwake, Amewadhibiti viumbe Wake wote na Ameijua idadi yao, hakuna yoyote miongono mawao mwenye kufichika na Yeye.

### الآية 19:95

> ﻿وَكُلُّهُمْ آتِيهِ يَوْمَ الْقِيَامَةِ فَرْدًا [19:95]

Na kila mtu, miongoni mwa viumbe, atamjia Mola wake, Siku ya Kiyama, hali ya kuwa hana mali wala watoto pamoja na yeye.

### الآية 19:96

> ﻿إِنَّ الَّذِينَ آمَنُوا وَعَمِلُوا الصَّالِحَاتِ سَيَجْعَلُ لَهُمُ الرَّحْمَٰنُ وُدًّا [19:96]

Hakika wale waliomuamini Mwenyezi Mungu, wakawafuata Mitume Wake na wakatenda mema kulingana na sheria Yake, Mwingi wa rehema Atatia katika nyoyo za waja Wake mahaba ya kuwapenda.

### الآية 19:97

> ﻿فَإِنَّمَا يَسَّرْنَاهُ بِلِسَانِكَ لِتُبَشِّرَ بِهِ الْمُتَّقِينَ وَتُنْذِرَ بِهِ قَوْمًا لُدًّا [19:97]

Hakika sisi tumeirahisisha hii Qur’ani katika ulimi wako wa Kiarabu, ewe Mtume, ili uwape bishara wachamungu, miongoni mwa wafuasi wako, na uwaonye kwayo wakanushaji wenye utesi sana kwa njia isiyofaa.

### الآية 19:98

> ﻿وَكَمْ أَهْلَكْنَا قَبْلَهُمْ مِنْ قَرْنٍ هَلْ تُحِسُّ مِنْهُمْ مِنْ أَحَدٍ أَوْ تَسْمَعُ لَهُمْ رِكْزًا [19:98]

Na mara nyingi tumewaangamiza ummah waliotangulia kabla ya watu wako, humuoni yoyote miongoni mwao na husikii sauti yao, basi hivyo ndivyo watakavyokuwa makafiri wa watu wako, tutawaangamiza kama tulivyowaangamiza waliotanguli kabla yao. Katika hii pana onyo na agizo la kuwaangamiza wakanushaji wenye ushindani wa ubatilifu.

## روابط ذات صلة

- [النص القرآني للسورة](https://quranpedia.net/surah/1/19.md)
- [كل تفاسير سورة مريم
](https://quranpedia.net/surah-tafsir/19.md)
- [ترجمات سورة مريم
](https://quranpedia.net/translations/19.md)
- [صفحة الكتاب: الترجمة السواحلية - عبد الله محمد وناصر خميس](https://quranpedia.net/book/27820.md)

---

زُر [Quranpedia.net](https://quranpedia.net/surah/1/19/book/27820) — موسوعة القرآن الكريم: التفاسير، الترجمات، التلاوات، والمواضيع.
