ﰅ
surah.translation
.
ﰡ
Je, ilikujia,ewe Mtume, habari ya Kiyama chenye vituko venye kuwaenea watu?
Nyuso za Makafiri, Siku hiyo, zitakuwa zimenyongeka kwa adhabu.
ﮆﮇ
ﰂ
Zishughulishie, zimechoka na kutaabika.
Zinachomwa kwa Moto wenye kuwaka kwa ukali.
Zitanyweshwa maji ya chemchemi yenye moto sana.
Watu wa Motoni hawatakuwa na chakula isipokuwa kinachotoka kwenye mti wa miba ilioshikana na chini. Ni kibaya sana chakula hiko na ni kichafu mno.
Hakimnoneshi mwenye kukila, awapo amekonda, wala hakimuondolei njaa, awapo na njaa.
Nyuso za Waumini, siku ya Kiyama, zitakuwa kwenye neema.
ﮤﮥ
ﰈ
Kwa kuwa zilijishughulisha ulimwenguni kumtii Mwenyezi Mungu na kuridhika na Akhera.
Zitakuwa kwenye Pepo ya daraja ya juu.
Hutasikia humo hata neno moja la upuuzi.
Ndani yake kuna chemchemi yenye kuteremka maji yake.
Ndani yake mna vitanda vilioangatika,
ﯙﯚ
ﰍ
na vikombe vilivyotayarishwa kwa wenye kunywa,
ﯜﯝ
ﰎ
na mito iliyopangwa, mmoja baada ya mwingine,
ﯟﯠ
ﰏ
na mazulia mengi yaliyotandikwa.
Kwani, hawa makafiri wenye kukanusha, hawaangalii ngamia namna walivyoumbwa kiajabu?
Na mbingu namna zlizoinuliwa juu kwa namna ya kupendeza?
Na milima namna iliyoimarishwa ukapatikana uthabiti na utulivu wa ardhi?
Na ardhi namna ilivyotandikwa na kutayarishwa?
Basi wawaidhie, ewe Mtume, wale wenye kupa nyongo yale uliyotumilizwa kwayo wala usihuzunike kwa kupa mgongo kwao.
Kwani wewe ni muwaidhiaji kwao, na si juu yako kuwalazimisha kuamini..
Lakini yule mwenye kuyapa mgongo makumbusho na mawaidha na akawa mkakamavu kwenye ukafiri wake,
Mwenyezi Mungu Atamuadhibu adhabu kali Motoni.
Hakika wao watarudi kwetu baada ya kufa.
Kisha ni juu yetu kuwalipa kwa waliyoyafanya.