رَبَّنَا لَا تَجۡعَلۡنَا فِتۡنَةٗ لِّلَّذِينَ كَفَرُواْ وَٱغۡفِرۡ لَنَا رَبَّنَآۖ إِنَّكَ أَنتَ ٱلۡعَزِيزُ ٱلۡحَكِيمُ
Mola wetu Mlezi! Usitufanyie mtihani kwa walio kufuru. Na tusamehe, Mola wetu Mlezi. Hakika Wewe ndiye Mwenye nguvu, Mwenye hikima.
Ali Muhsin Al - Swahili translation
Mola wetu! Usitufanye ni mtihani wa wale waliokukanusha wewe, kwa kutuadhibu au kuwapa nguvu makafiri juu yetu wakatufitini kwa kutuepusha na Dini yetu au wakawa na nguvu juu yetu wakafitinika kwa hilo na hapo waseme, «Lau hawa wangalikuwa kwenye haki haingaliwapata adhabu hii,» na wazidi ukafiri. Na utufinikie dhambi zetu kwa kutusamehe, ewe Mola wetu! Hakika wewe ni Mshindi Asiyekuwa na mwenye kushindana Naye, Mwingi wa hekima katika maneno Yake na matendo Yake.
الترجمة السواحلية - عبد الله محمد وناصر خميس