ﯹ
surah.translation
.
ﰡ
Kishampitia binadamu kipindi kirefa cha wakati kabla hajapulizwa roho ambapo hakuwa ni kita kinachotajika wala haijulikani athari yake.
Sisi tumemuumba binadamu kutokana na tone la manii la mchanganyiko wa maji ya mwanamume na maji ya mwanamke, ili tumtahini kwa lazima za kisheria baadaye, hivyo basi tumfanya ni mwenye masikio ya kusikia na macho ya kuonea, apate kuzisikia aya na kuziona dalili.
Sisi tumembainishia na kumfahamisha njia ya uongofu na upotevu na wema na ubaya ili awe ima ni mwenye kuamini na kushukuru. Au awe ni mwenye kukanusha na kukataa.
Sisi Tumewaandalia wakanushaji pingu za chuma za kuifunga miguu yao na minyororo ya kufungiwa mikono yao hadi shingo zao na moto ambao watachomwa nao.
Hakika watu wa utiifu na ukweli wa Imani wanaotekeleza haki za Mwenyezi Mungu, watakunywa, Siku ya Kiyama, kutoka kwenye kikombe ambacho ndani yake mna Pombe lililochanganywa na aina bora kabisa ya harufu nzuri, nayo ni maji ya kafuri.
Kinywaji hiki kilichochanganywa na kafuri, ni chemchemi wanayokunywa waja wa Mwenyezi Mungu, wanaitumia na kuipitisha wanavyotaka mapitisho mazuri.
Hao walikuwa huko duniani wanatekeleza kile walichojilazimisha nafsi zao cha utiifu kwa Mwenyezi Mungu, na wakiogopa mateso ya Mwenyezi Mungu, Siku ya Kiyama, ambayo madhara yake ni hatari na ubaya ni wenye kusambaa na kuenea kwa watu isipokuwa wale ambao Mwenyezi Mungu Amewarehemu.
Na wanalisha chakula, pamoja na kuwa wanakipenda na kukihitajia, kumpa fukara asiyeweza kuchuma, asiyemiliki chochote katika vitu vya kilimwengu, na kumpa mtoto aliyefiliwa na babake kabla ya kubaleghe na asiye na mali, na kumpa mtu aliyetekwa vitani miongoni mwa washirikina na wengineo,
na huku wanasema katika nafsi zao, «Hakika sisi tunawafanyia wema kwa kutafuta radhi za Mwenyezi Mungu na kutaka malipo yake. Hatutaki badala wala hatukusudii kushukuriwa wala kusifiwa na nyinyi.
Kwa kweli, sisi tunaiogopa, kutoka kwa Mola wetu, Siku ngumu ambayo ndani yake nyuso zitakunjana na mapaji yatasinyaa kutokana na mambo yake mazito na vituko vyake vikubwa.
Basi hao Mwenyezi Mungu Atawaokoa na shida za Siku hiyo na Atawapa uzuri na mwangaza katika nyuso zao na furaha ndani ya nyoyo zao,
na Atawalipa, kwa kuvumilia kwao duniani juu ya utiifu, Pepo iliyo kubwa ambayo kutoka humo watakula wanachokitaka na watavaa humo hariri nyororo,
hali ya kuwa wametegemea juu ya vitanda vilivyopambwa kwa nguo na pazia za fahari. Hawataona humo joto la jua wala ukali wa baridi.
Na karibu nao, kutakuwa na miti ya Pepo yenye kuwafinika ambayo wamerahisishiwa kuyachuma matunda yake.
Watawazunguka wao watumishi wakiwa na vyombo vya vyakula vya fedha, na vikombe vya vinywaji vya ukoa,
ukowa wa fedha, ambavyo wanyweshaji wamevima kadiri ya watakavyotamani wenye kunywa, haviongezeki wala havipungui.
Na watu wema hawa watanyweshwa Peponi kikombe kilichijazwa Pombe iliyochanganywa na tangawizi,
watakunwa kutoka kwenye chemchemi iliyoko Peponi inayoitwa Salsabīl, kwa kuwa kinywaji chake kina usalama na kuwa kina ulaini na ladha ya kupendeza.
Na watawazunguka wema hawa wakiwatumikia wavulana wenye hali moja ya kudumu, ukiwaona utawadhania, kwa uzuri wao na usafi wa rangi zao na mng’aro wa nyuso zao, kuwa ni lulu iliyotenganishwa inayong’ara.
Na utazamapo mahali popote katika Pepo utaona starehe isiyosifika na ufalme mkubwa uliop mkunjufu usiosiokuwa na mwisho.
Juu ya miili yao pana nguo zilizoipamba, ambazo sehemu zake za ndani kuna hariri nyembamba ya rangi ya kijani, na nje yake kuna hariri nene. Na miongoni mwa mapambo watakayovishwa ni makuku ya fedha. Na Mola wao Atawanywesha, juu ya sterehe hizo, kinywaji kisicho na uchafu wala rojo.
Na wataambiwa, «Hakika nyinyi mmetayarishiwa haya yakiwa ni badala ya matendo yenu mema, na matendo yenu duniani yalikuwa ni yenye kukubaliwa na kuridhiwa na Mwenyezi Mungu.»
Hakika sisi tumekuteremshia Qur’ani, ewe Mtume, materemsho yanayotoka kwetu, ili uwakumbushe watu yale yaliyomo ndani ya maagizo mema, matahadharisho ya ubaya, malipo mazuri na mateso.
Basi yavumilie maamuzi ya Mola Wako Aliyokupangia na uyakubali, na usonge mbele kufuata maamrisho yake ya Kidini, na usiwatii washirikina waliovama kwenye matamanio au waliokolea kwenye ukafiri na upotevu,
na uendelee kutaja jina la Mola wako na kumuomba mwanzo wa mchana na mwisho wake.
Na wakati wa usiku, mnyenyekee Mola wako na umswalie na umuabudu kipindi kirefu cha usiku.
Kwa hakika hawa washirikina wanaupenda ulimwengu na wanaushughulikia, na wanakuacha nyuma ya migongo yao kule kufanya matendo ya kuwafaa Akhera na kuwaokoa katika Siku yenye shida kubwa.
Sisi Ndio tuliowaumba na tukalipa uthabiti umbo lao. Na tunapotaka tunawaangamiza na kuwaleta watu walio watiifu zaidi wa Mwenyezi Mungu kuliko wao.
Hakika ndani ya sura hii, kwa yaliyomo ya kuvutia na kuogopesha, ya kuahidi mema na kuonya mabaya, kuna mawaidha kwa viumbe wote. Basi mwenye kujitakia wema nafsi yake ya duniani na Akhera, na ashike njia ya Imani na uchamungu itakayomfikisha kwenye msamaha wa Mwenyezi Mungu na radhi Zake.
Na hamtataka jambo lolote miongoni mwa mambo isipokuwa kwa makadirio ya Mwenyezi Mungu na matakwa Yake. Hakika Mwenyezi Mungu ni Mjuzi wa hali za viumbe Vyake, ni Mwingi wa hekima katika uendeshaji na utengezaji Wake.
Anamuingiza Anayemtaka miongoni mwa waja Wake katika rehema Yake na radhi Yake, na wao ni wale walioamini. Na Amewaandalia madhalimu waliokiuka mipaka ya Mwenyezi Mungu adhabu yenye kuumiza.