يَٰٓأَيُّهَا ٱلَّذِينَ ءَامَنُواْ لَا تَأۡكُلُواْ ٱلرِّبَوٰٓاْ أَضۡعَٰفࣰا مُّضَٰعَفَةࣰۖ وَٱتَّقُواْ ٱللَّهَ لَعَلَّكُمۡ تُفۡلِحُونَ ١٣٠
Al-Imran 3:130
سورة آل عمران
Madina
Aya: 130/200
Ukurasa 66
-
Ali Muhsin Al - Swahili translation
Enyi mlio amini! Msile riba mkizidisha juu kwa juu, na mcheni Mwenyezi Mungu ili mpate kufanikiwa. -
Abdullah Muhammad & Nassir Khamis
الترجمة السواحلية - عبد الله محمد وناصر خميس
Enyi mliomuamini Mwenyezi Mungu na Mtume Wake na mkazifuata Sheria Zake kivitendo, tahadharini na aina zote za riba na msichukue katika mkopo zaidi ya rasilmali zenu, hata kama ni kidogo. Basi itakuwaje iwapo ziada hiyo itaongezeka kila ufikapo muda wa kulipa deni? Na muogopeni Mwenyezi Mungu kwa kujilazimisha kufuata Sheria Zake ili mpate kufaulu duniani na Akhera.
Al-Imran 3:130
Inapakia kisomo…
0:00