قُلۡ أَطِيعُواْ ٱللَّهَ وَٱلرَّسُولَۖ فَإِن تَوَلَّوۡاْ فَإِنَّ ٱللَّهَ لَا يُحِبُّ ٱلۡكَٰفِرِينَ ٣٢
Al-Imran 3:32
سورة آل عمران
Madina
Aya: 32/200
Ukurasa 54
-
Ali Muhsin Al - Swahili translation
Sema: Mt'iini Mwenyezi Mungu na Mtume. Na wakigeuka basi Mwenyezi Mungu hawapendi makafiri. -
Abdullah Muhammad & Nassir Khamis
الترجمة السواحلية - عبد الله محمد وناصر خميس
Sema, ewe Mtume, «Mtiini Mwenyezi Mungu kwa kufuata Kitabu Chake, na mtiini Mtume kwa kufuata mwenendo wake wakati wa uhai wake na baada ya kufa kwake.Wakiwa watakupa mgongo na kukamaa kwenye ukafiri na upotevu walionao, wao hawatakuwa wanastahili mapenzi ya Mwenyezi Mungu. Kwani Mwenyezi Mungu Hawapendi makafiri.
Al-Imran 3:32
Inapakia kisomo…
0:00