أَمۡ يَقُولُونَ ٱفۡتَرَىٰهُۖ قُلۡ إِنِ ٱفۡتَرَيۡتُهُۥ فَلَا تَمۡلِكُونَ لِي مِنَ ٱللَّهِ شَيۡـًٔاۖ هُوَ أَعۡلَمُ بِمَا تُفِيضُونَ فِيهِۚ كَفَىٰ بِهِۦ شَهِيدَۢا بَيۡنِي وَبَيۡنَكُمۡۖ وَهُوَ ٱلۡغَفُورُ ٱلرَّحِيمُ ٨
Al-Ahqaf 46:8
سورة الأحقاف
Makka
Aya: 8/35
Ukurasa 503
-
Ali Muhsin Al - Swahili translation
Au wanasema: Ameizua mwenyewe! Sema: Ikiwa nimeizua mimi, basi nyinyi hamwezi kunifaa chochote mbele ya Mwenyezi Mungu. Yeye anajua zaidi hayo mnayo ropokwa; anatosha kuwa shahidi baina yangu na nyinyi. Na Yeye ndiye Mwenye kusamehe, Mwenye kurehemu. -
Abdullah Muhammad & Nassir Khamis
الترجمة السواحلية - عبد الله محمد وناصر خميس
Au je wanasema hawa washirikina kwamba Muhammad ameizua Qur’ani? Waambie, ewe mtume, “Iwapo mimi nimemzulia Mwenyezi Mungu hii Qur’ani, basi nyinyi hamuwezi kunikinga mimi na adhabu ya Mwenyezi Mungu kitu chochote Akiwa atanitesa kwa hilo. Yeye, kutakasika ni Kwake, ni Mjuzi zaidi wa kile mnachokisema juu ya hii Qur’ani kuliko kitu chochote kingine. Inatosha kuwa Mwenyezi Mungu ni Shahidi juu yangu mimi na nyinyi, na Yeye Ndiye Mwingi wa msamaha kwa waja Wake, ni Mwingi wa rehema kwa waja Wake Waumini.”
Al-Ahqaf 46:8
Inapakia kisomo…
0:00