وَلَا تُطِعِ ٱلۡكَٰفِرِينَ وَٱلۡمُنَٰفِقِينَ وَدَعۡ أَذَىٰهُمۡ وَتَوَكَّلۡ عَلَى ٱللَّهِۚ وَكَفَىٰ بِٱللَّهِ وَكِيلࣰا ٤٨
AlAhzab 33:48
سورة الأحزاب
Madina
Aya: 48/73
Ukurasa 424
-
Ali Muhsin Al - Swahili translation
Wala usiwat'ii makafiri na wanaafiki, na usijali udhia wao. Nawe mtegemee Mwenyezi Mungu. Na Mwenyezi Mungu anatosha kuwa Mtegemewa. -
Abdullah Muhammad & Nassir Khamis
الترجمة السواحلية - عبد الله محمد وناصر خميس
Na usilitii, ewe Nabii, neno la kafiri au mnafiki na uuache udhia wao, na hilo lisikuzuie kufikisha ujumbe, na kuwa na imani na Mwenyezi Mungu katika mambo yako yote, na umtegemee Yeye, kwani Yeye Atakutosheleza yanayokutia hamu miongoni mwa mambo yote ya ulimwengu na Akhera.
AlAhzab 33:48
Inapakia kisomo…
0:00