لِيَمِيزَ ٱللَّهُ ٱلۡخَبِيثَ مِنَ ٱلطَّيِّبِ وَيَجۡعَلَ ٱلۡخَبِيثَ بَعۡضَهُۥ عَلَىٰ بَعۡضࣲ فَيَرۡكُمَهُۥ جَمِيعࣰا فَيَجۡعَلَهُۥ فِي جَهَنَّمَۚ أُوْلَٰٓئِكَ هُمُ ٱلۡخَٰسِرُونَ ٣٧
Al-Anfal 8:37
سورة الأنفال
Madina
Aya: 37/75
Ukurasa 181
-
Ali Muhsin Al - Swahili translation
Ili Mwenyezi Mungu apate kuwa pambanua walio waovu na walio wema, na kuwaweka waovu juu ya waovu wengine, na kuwarundika wote pamoja, na kuwatupa katika Jahannam. Hao ndio walio khasirika. -
Abdullah Muhammad & Nassir Khamis
الترجمة السواحلية - عبد الله محمد وناصر خميس
Mwenyezi Mungu Atawakusanya na Atawatweza hawa ambao walimkanusha Mola wao na wakatoa mali yao kuwazuia watu kumuamini Mwenyezi Mungu na kuzuia njia Yake isifuatwe, ili Mwenyezi Mungu, Aliyetukuka, Apate kukipambanua kichafu na kizuri, na ili Ayakusanye Mwenyezi Mungu mali ya haramu, yaliyotumiwa kuwazuia watu na dini ya Mwenyezi Mungu, Ayaweke baadhi yake juu ya mengine yawe yamekusanyikana na kupandana kisha Ayatie kwenye Moto wa Jahanamu. Makafiri hawa ndio wenye kupata hasara duniani na Akhera.
Al-Anfal 8:37
Inapakia kisomo…
0:00