أَوَلَمۡ يَرَوۡاْ أَنَّا جَعَلۡنَا حَرَمًا ءَامِنࣰا وَيُتَخَطَّفُ ٱلنَّاسُ مِنۡ حَوۡلِهِمۡۚ أَفَبِٱلۡبَٰطِلِ يُؤۡمِنُونَ وَبِنِعۡمَةِ ٱللَّهِ يَكۡفُرُونَ ٦٧
Al-'Ankabut 29:67
سورة العنكبوت
Makka
Aya: 67/69
Ukurasa 404
-
Ali Muhsin Al - Swahili translation
Je! Hawaoni ya kwamba tumeifanya nchi takatifu ina amani, na hali watu wengine wananyakuliwa kote kwa majirani zao? Je! Wanaamini upotovu, na neema za Mwenyezi Mungu wanazikataa? -
Abdullah Muhammad & Nassir Khamis
الترجمة السواحلية - عبد الله محمد وناصر خميس
Kwani hawakushuhudia makafiri wa Makkah kwamba Mwenyezi Mungu Amewawekea Makkah kuwa ni mahali patakatifu penye amani, watu wake wanapata amani humo ya nafsi zao na mali zao, hali watu walio pambizoni mwake, nje ya eneo takatifu, wananyakuliwa hawana amani? Je, ni ushirikina wanaouamini na ni neema ya Mwenyezi Mungu Aliyowahusu wao nayo, wanayoikanusha, wakawa hawamuabudu Yeye, Peke Yake, bila mwingine?
Al-'Ankabut 29:67
Inapakia kisomo…
0:00