إِنَّآ أَرۡسَلۡنَٰكَ بِٱلۡحَقِّ بَشِيرࣰا وَنَذِيرࣰاۖ وَلَا تُسۡـَٔلُ عَنۡ أَصۡحَٰبِ ٱلۡجَحِيمِ ١١٩
Al-Baqarah 2:119
سورة البقرة
Madina
Aya: 119/286
Ukurasa 18
-
Ali Muhsin Al - Swahili translation
Hakika Sisi tumekutuma kwa Haki uwe mbashiri, na mwonyaji. Na wala hutaulizwa juu ya watu wa Motoni. -
Abdullah Muhammad & Nassir Khamis
الترجمة السواحلية - عبد الله محمد وناصر خميس
Sisi tumekutumiliza, ewe Mtume, kwa Dini ya haki iliyotiliwa nguvu kwa hoja na miujiza. Basi ifikishe kwa watu, pamoja na kuwapa Waumini bishara ya kheri ya dunia na ya Akhera, na kuwatisha wakaidi na adhabu ya Mwenyezi Mungu inayowangojea. Na baada ya kufikisha ujumbe, hutaulizwa juu ya ukafiri wa wenye kukukanusha. Wao wataingia Motoni, Siku ya Kiyama, wala hawatatoka humo.
Al-Baqarah 2:119
Inapakia kisomo…
0:00