ٱلَّذِينَ ءَاتَيۡنَٰهُمُ ٱلۡكِتَٰبَ يَعۡرِفُونَهُۥ كَمَا يَعۡرِفُونَ أَبۡنَآءَهُمۡۖ وَإِنَّ فَرِيقࣰا مِّنۡهُمۡ لَيَكۡتُمُونَ ٱلۡحَقَّ وَهُمۡ يَعۡلَمُونَ ١٤٦
Al-Baqarah 2:146
سورة البقرة
Madina
Aya: 146/286
Ukurasa 23
-
Ali Muhsin Al - Swahili translation
Wale tulio wapa Kitabu wanayajua haya kama wanavyo wajua watoto wao; na kuna kikundi katika wao huificha haki na hali wanajua. -
Abdullah Muhammad & Nassir Khamis
الترجمة السواحلية - عبد الله محمد وناصر خميس
Wale Tuliowapa Taurati na Injili miongoni mwa wanavyuoni wa Kiyahudi na wajuzi wa Kinaswara wanajua ya kwamba Muhammad, rehema ya Mwenyezi Mungu na amani zimshukie, ni mjumbe wa Mwenyezi Mungu, kwa sifa zake zilizotajwa katika vitabu vyao, kama vile wanavyowajuwa wana wao. Na hakika kuna kundi kati yao wanaificha haki na wao wanaujuwa ukweli wake na kuwa sifa zake zimethibiti.
Al-Baqarah 2:146
Inapakia kisomo…
0:00