وَمِنَ ٱلنَّاسِ مَن يُعۡجِبُكَ قَوۡلُهُۥ فِي ٱلۡحَيَوٰةِ ٱلدُّنۡيَا وَيُشۡهِدُ ٱللَّهَ عَلَىٰ مَا فِي قَلۡبِهِۦ وَهُوَ أَلَدُّ ٱلۡخِصَامِ ٢٠٤
Al-Baqarah 2:204
سورة البقرة
Madina
Aya: 204/286
Ukurasa 32
-
Ali Muhsin Al - Swahili translation
Na katika watu yupo yule ambaye maneno yake kwa maisha ya kidunia hukufurahisha; naye humshuhudisha Mwenyezi Mungu kwa yaliyomo moyoni mwake, na hali yeye ndiye mkubwa wa ukhasimu. -
Abdullah Muhammad & Nassir Khamis
الترجمة السواحلية - عبد الله محمد وناصر خميس
Na baadhi ya watu miongoni mwa wanafiki yanakuvutia, ewe Mtume, maneno yake yaliyo fasaha ambayo kwayo anataka fungu la hadhi za duniani, si za Akhera, na anaapa huku akimshuhudisha Mwenyezi Mungu yaliyo moyoni mwake ya kuupenda Uislamu, hali ya kuwa yeye ana uadui na utesi mkubwa juu ya Uislamu na Waislamu. Huo ni upeo wa ujasiri juu ya Mwenyezi Mungu.
Al-Baqarah 2:204
Inapakia kisomo…
0:00