۞ أَفَتَطۡمَعُونَ أَن يُؤۡمِنُواْ لَكُمۡ وَقَدۡ كَانَ فَرِيقࣱ مِّنۡهُمۡ يَسۡمَعُونَ كَلَٰمَ ٱللَّهِ ثُمَّ يُحَرِّفُونَهُۥ مِنۢ بَعۡدِ مَا عَقَلُوهُ وَهُمۡ يَعۡلَمُونَ ٧٥
Al-Baqarah 2:75
سورة البقرة
Madina
Aya: 75/286
Ukurasa 11
-
Ali Muhsin Al - Swahili translation
Mnatumai watakuaminini na hali baadhi yao walikuwa wakisikia maneno ya Mwenyezi Mungu, kisha wakayabadili baada ya kuwa wameyafahamu, na hali wanajua? -
Abdullah Muhammad & Nassir Khamis
الترجمة السواحلية - عبد الله محمد وناصر خميس
Enyi waislamu! Kwani mumesahau vitendo vya Wana wa Isrāīl, ndipo nafsi zenu zikawa na tamaa kuwa Mayahudi wataiamini dini yenu? Wanavyuoni wao walikuwa wakisikia maneno ya Mwenyezi Mungu ya Taurati, kisha wakiyapotoa kwa kuyageuza na kuyapa maana yasiyo sahihi baada ya kuyafahamu maana yake ya kweli, au kwa kuyageuza matamshi yake, hali wanajua kuwa wao wanayapotoa maneno ya Mwenyezi Mungu kwa kusudi na urongo.
Al-Baqarah 2:75
Inapakia kisomo…
0:00