مَن كَانَ عَدُوࣰّا لِّلَّهِ وَمَلَٰٓئِكَتِهِۦ وَرُسُلِهِۦ وَجِبۡرِيلَ وَمِيكَىٰلَ فَإِنَّ ٱللَّهَ عَدُوࣱّ لِّلۡكَٰفِرِينَ ٩٨
Al-Baqarah 2:98
سورة البقرة
Madina
Aya: 98/286
Ukurasa 15
-
Ali Muhsin Al - Swahili translation
Aliye kuwa adui wa Mwenyezi Mungu na Malaika wake na Mitume wake na Jibril na Mikail, basi hakika Mwenyezi Mungu ni adui wa makafiri. -
Abdullah Muhammad & Nassir Khamis
الترجمة السواحلية - عبد الله محمد وناصر خميس
Mwenye kumfanyia uadui Mwenyezi Mungu, Malaika Wake, Wajumbe Wake ambao ni Malaika au binadamu, hasahasa Malaika wawili: Jibrili na Mikaili, huwa amemfanyia uadui Mwenyezi Mungu. Sababu Mayahudi walidai kwamba Jibrili ni adui wao na Mikaili ni rafiki yao. Mwenyezi Mungu Akawajulisha kwamba mwenye kuwa adui wa mmoja katika wao huwa ni adui wa Mwengine na pia ni adui wa Mwenyezi Mungu. Kwani Mwenyezi Mungu ni adui wa wenye kuyakanusha yale aliyoyateremsha kwa Mtume wake Muhammad, rehema na amani zimshukie.
Al-Baqarah 2:98
Inapakia kisomo…
0:00