هُوَ ٱلَّذِيٓ أَنزَلَ ٱلسَّكِينَةَ فِي قُلُوبِ ٱلۡمُؤۡمِنِينَ لِيَزۡدَادُوٓاْ إِيمَٰنࣰا مَّعَ إِيمَٰنِهِمۡۗ وَلِلَّهِ جُنُودُ ٱلسَّمَٰوَٰتِ وَٱلۡأَرۡضِۚ وَكَانَ ٱللَّهُ عَلِيمًا حَكِيمࣰا ٤
Al-Fath 48:4
سورة الفتح
Madina
Aya: 4/29
Ukurasa 511
-
Ali Muhsin Al - Swahili translation
Yeye ndiye aliye teremsha utulivu katika nyoyo za Waumini ili wazidi Imani juu ya Imani yao. Na Mwenyezi Mungu ndiye mwenye majeshi ya mbingu na ardhi. Na Mwenyezi Mungu ni Mwenye ujuzi, Mwenye hikima - -
Abdullah Muhammad & Nassir Khamis
الترجمة السواحلية - عبد الله محمد وناصر خميس
Yeye Ndiye Mwenyezi Mungu Aliyeteremsha utulivu ndani ya nyoyo za wenye kumuamini Mwenyezi Mungu na Mtume Wake katika siku ya Ḥudaybiyah zikatulia na yakini ikajidhatititi ndani ya hizo nyoyo, ili wazidi kumuamini Mwenyezi Mungu na kumfuata Mtume Wake pamoja na kuamini kwao na kufuata kwao. Na Mwenyezi Mungu, Aliyetakasika na kutukuka, Ana askari wa mbinguni na ardhini, Anawanusuru kwa askari hao waja Wake Waumini. Na Mwenyezi Mungu ni Mjuzi sana wa maslahi ya viumbe Vyake, ni Mwingi wa hekima katika uendeshaji mambo Wake na utengezaji Wake.
Al-Fath 48:4
Inapakia kisomo…
0:00