۞ ذَٰلِكَۖ وَمَنۡ عَاقَبَ بِمِثۡلِ مَا عُوقِبَ بِهِۦ ثُمَّ بُغِيَ عَلَيۡهِ لَيَنصُرَنَّهُ ٱللَّهُۚ إِنَّ ٱللَّهَ لَعَفُوٌّ غَفُورࣱ ٦٠
Al-Hajj 22:60
سورة الحج
Madina
Aya: 60/78
Ukurasa 339
-
Ali Muhsin Al - Swahili translation
Ndio namna hivi. Na anaye lipiza mfano wa alivyo adhibiwa, kisha akadhulumiwa, basi hapana shaka Mwenyezi Mungu atamsaidia. Hakika Mwenyezi Mungu ni Msamehevu Mwenye maghfira. -
Abdullah Muhammad & Nassir Khamis
الترجمة السواحلية - عبد الله محمد وناصر خميس
Hilo ni jambo tulilokusimulia la kuwatia Peponi waliogura(katika njia ya Mwenyezi Mungu), na mwenye kufanyiwa uadui na kuonewa basi yeye ameruhusiwa kupambana na huyo mhalifu kwa kitendo kama chake, na atakuwa hana makosa. Na akirudi yule mhalifu kumuonea na akafanya udhalimu, basi Mwenyezi Mungu Atampa ushindi yule mdhulumiwa aliyeonewa, kwani haifai afanyiwe uadui kwa kuwa amejilipizia. Hakika Mwenyezi Mungu ni Msamehefu ni Mwingi wa kughofiria, Anasamehe dhambi za wenye kukosea, hawafanyii haraka kuwatesa na anazifinika dhambi zao.
Al-Hajj 22:60
Inapakia kisomo…
0:00