وَلَقَدۡ ءَاتَيۡنَا مُوسَىٰ تِسۡعَ ءَايَٰتِۭ بَيِّنَٰتࣲۖ فَسۡـَٔلۡ بَنِيٓ إِسۡرَٰٓءِيلَ إِذۡ جَآءَهُمۡ فَقَالَ لَهُۥ فِرۡعَوۡنُ إِنِّي لَأَظُنُّكَ يَٰمُوسَىٰ مَسۡحُورࣰا ١٠١
Al-Isra 17:101
سورة الإسراء
Makka
Aya: 101/111
Ukurasa 292
-
Ali Muhsin Al - Swahili translation
Na kwa yakini tulimpa Musa ishara tisa zilizo wazi. Waulize Wana wa Israili alipo wafikia, na Firauni akawaambia: Hakika mimi nakuona wewe Musa umerogwa! -
Abdullah Muhammad & Nassir Khamis
الترجمة السواحلية - عبد الله محمد وناصر خميس
Na hakika tulimpa Mūsā miujiza tisa iliyo waziwazi, yenye kutolea ushahidi wa ukweli wa unabii wake, nayo ni fimbo, mkono, ukame, upungufu wa matunda, mafuriko, nzige, chawa, vyura na damu. Basi waulize Mayahudi, ewe Mtume, suala la kuthibitisha, pale Mūsā alipowajia mababu zao na miujiza iliyo wazi, Fir'awn akasema kumwambia Mūsā, «Mimi nadhani, ewe Mūsā, kwamba wewe ni mchawi uliodanganywa na kutekwa akili yako kwa vitendo hivyo vya ajabu unavyovileta.»
Al-Isra 17:101
Inapakia kisomo…
0:00