وَبِٱلۡحَقِّ أَنزَلۡنَٰهُ وَبِٱلۡحَقِّ نَزَلَۗ وَمَآ أَرۡسَلۡنَٰكَ إِلَّا مُبَشِّرࣰا وَنَذِيرࣰا ١٠٥
Al-Isra 17:105
سورة الإسراء
Makka
Aya: 105/111
Ukurasa 293
-
Ali Muhsin Al - Swahili translation
Na kwa Haki tumeiteremsha, na kwa Haki imeteremka. Na hatukukutuma ila uwe mbashiri na mwonyaji. -
Abdullah Muhammad & Nassir Khamis
الترجمة السواحلية - عبد الله محمد وناصر خميس
Na tumemteremshia Muhammad, rehema ya Mwenyezi Mungu na amani zimshukiye, hii Qur’ani ili kuwaamrisha waja, kuwakataza, kuwalipa mema na kuwaadhibu; na imeteremka kwa ukweli, uadilifu na utunzi isibadilishwe na isigeuzwe. Na hatukukutumiliza wewe, ewe Mtume, isipokuwa ni uwabashirie Pepo waliotii na uwatishe na Moto walioasi na kukanusha.
Al-Isra 17:105
Inapakia kisomo…
0:00