وَنُنَزِّلُ مِنَ ٱلۡقُرۡءَانِ مَا هُوَ شِفَآءࣱ وَرَحۡمَةࣱ لِّلۡمُؤۡمِنِينَ وَلَا يَزِيدُ ٱلظَّٰلِمِينَ إِلَّا خَسَارࣰا ٨٢
Al-Isra 17:82
سورة الإسراء
Makka
Aya: 82/111
Ukurasa 290
-
Ali Muhsin Al - Swahili translation
Na tunateremsha katika Qur'ani yaliyo ni matibabu na rehema kwa Waumini. Wala hayawazidishii madhaalimu ila khasara. -
Abdullah Muhammad & Nassir Khamis
الترجمة السواحلية - عبد الله محمد وناصر خميس
Na tunateremsha miongoni mwa aya za Qur’ani yanayopoza magonjwa ya nyoyo kama shaka , unafiki na ujinga, na yanayopoza miili kwa kujizungua nayo, na yanayokuza Imani ambayo ni sababu ya kufaulu kupata rehema ya Mwenyezi Mungu. Na hii Qur’ani haiwaongezei makafiri wanapoisikia isipokua ukafiri na upotevu, kwa kuikanusha kwao na kutoiamini.
Al-Isra 17:82
Inapakia kisomo…
0:00