وَسَخَّرَ لَكُم مَّا فِي ٱلسَّمَٰوَٰتِ وَمَا فِي ٱلۡأَرۡضِ جَمِيعࣰا مِّنۡهُۚ إِنَّ فِي ذَٰلِكَ لَأٓيَٰتࣲ لِّقَوۡمࣲ يَتَفَكَّرُونَ ١٣
Al-Jathiya 45:13
سورة الجاثية
Makka
Aya: 13/37
Ukurasa 499
-
Ali Muhsin Al - Swahili translation
Na amefanya vikutumikieni vilivyomo mbinguni na vilivyomo katika ardhi, vyote vimetoka kwake. Hakika katika hayo zimo Ishara kwa watu wanao fikiri. -
Abdullah Muhammad & Nassir Khamis
الترجمة السواحلية - عبد الله محمد وناصر خميس
Na Akawadhalilishia kila kilichoko mbinguni miongoni mwa jua , mwezi na nyota, na kila kilicho ardhini miongoni mwa wanyama, miti, majahazi na visiokuwa hivyo kwa ajili ya maslahi yenu. Neema zote hizi ni vipaji Alizowaneemesha nazo Mwenyezi Mungu Peke Yake na fadhila inayotoka Kwake Aliyowafadhili nayo. Basi Yeye Peke Yake muabuduni, na msimfanye yoyote kuwa ni mshirika Wake. Hakika katika vitu vile Alivyowadhalilishia Mwenyezi Mungu kuna alama na dalili juu ya upweke wa Mwenyezi Mungu kwa watu wenye kuzitia akilini aya za Mwenyezi Mungu, hoja Zake na dalili Zake, wakazizingatia.
Al-Jathiya 45:13
Inapakia kisomo…
0:00