ذَٰلِكُم بِأَنَّكُمُ ٱتَّخَذۡتُمۡ ءَايَٰتِ ٱللَّهِ هُزُوࣰا وَغَرَّتۡكُمُ ٱلۡحَيَوٰةُ ٱلدُّنۡيَاۚ فَٱلۡيَوۡمَ لَا يُخۡرَجُونَ مِنۡهَا وَلَا هُمۡ يُسۡتَعۡتَبُونَ ٣٥
Al-Jathiya 45:35
سورة الجاثية
Makka
Aya: 35/37
Ukurasa 502
-
Ali Muhsin Al - Swahili translation
Hayo ni kwa sababu nyinyi mlizifanyia mzaha Aya za Mwenyezi Mungu; na maisha ya dunia yakakudanganyeni. Basi leo hawatatolewa humo wala hao hawatakubaliwa udhuru wao. -
Abdullah Muhammad & Nassir Khamis
الترجمة السواحلية - عبد الله محمد وناصر خميس
«Haya yaliyowafika ya adhabu ya Mwenyezi Mungu ni kwa sababu ya kuwa nyinyi mlizifanya aya za Mwenyezi Mungu na hoja Zake kuwa shere na mchezo, na likawadanganya nyinyi pambo la uhai wa kilimwengu.» Basi Leo hawatatolewa Motoni wala hawatarudishwa ulimwenguni ili watubie na wafanye mema.
Al-Jathiya 45:35
Inapakia kisomo…
0:00