وَعُرِضُواْ عَلَىٰ رَبِّكَ صَفࣰّا لَّقَدۡ جِئۡتُمُونَا كَمَا خَلَقۡنَٰكُمۡ أَوَّلَ مَرَّةِۭۚ بَلۡ زَعَمۡتُمۡ أَلَّن نَّجۡعَلَ لَكُم مَّوۡعِدࣰا ٤٨
Al-Kahf 18:48
سورة الكهف
Makka
Aya: 48/110
Ukurasa 299
-
Ali Muhsin Al - Swahili translation
Na wakahudhurishwa mbele ya Mola wako Mlezi kwa safu (wakaambiwa): Mmetujia kama tulivyo kuumbeni mara ya kwanza! Bali mlidai kwamba hatutakuwekeeni miadi. -
Abdullah Muhammad & Nassir Khamis
الترجمة السواحلية - عبد الله محمد وناصر خميس
Na hapo watahudhurishwa wote kwa Mola wako wakiwa wamejipanga safu, hakuna yoyote kati yao anayefichwa, na hapo Awaambie «Tumewafufua na mumetujia mkiwa peke yenu, hakuna mali pamoja na nyinyi wala watoto, kama vile tulivyowaumba mara ya kwanza. Bali mlifikiria kwamba hatutawaekea nyinyi wakati wa kuwafufua na kuwalipa kwa matendo yenu.»
Al-Kahf 18:48
Inapakia kisomo…
0:00