۞ وَٱتۡلُ عَلَيۡهِمۡ نَبَأَ ٱبۡنَيۡ ءَادَمَ بِٱلۡحَقِّ إِذۡ قَرَّبَا قُرۡبَانࣰا فَتُقُبِّلَ مِنۡ أَحَدِهِمَا وَلَمۡ يُتَقَبَّلۡ مِنَ ٱلۡأٓخَرِ قَالَ لَأَقۡتُلَنَّكَۖ قَالَ إِنَّمَا يَتَقَبَّلُ ٱللَّهُ مِنَ ٱلۡمُتَّقِينَ ٢٧
Al-Ma'idah 5:27
سورة المائدة
Madina
Aya: 27/120
Ukurasa 112
-
Ali Muhsin Al - Swahili translation
Na wasomee khabari za wana wawili wa Adam kwa kweli. Walipo toa mhanga, ukakubaliwa wa mmoja wao, na wa mwengine haukukubaliwa. Akasema: Nitakuuwa. Akasema mwengine: Mwenyezi Mungu huwapokelea wachamngu. -
Abdullah Muhammad & Nassir Khamis
الترجمة السواحلية - عبد الله محمد وناصر خميس
Wasimulie, ewe Mtume, Wana wa Isrāīl habari ya wana wawili wa Ādam, Qābīl na Hābīl, nayo ni habari ya kweli, alipotoa kila mmoja wao sadaka, nayo ni ile inayotolewa ili kujisogeza karibu kwa Mwenyezi Mungu, Aliyetukuka. Hapo Mwenyezi Mungu Aliikubali sadaka ya Hābīl kwa kuwa alikuwa mcha-Mungu, na Hakuikubali sadaka ya Qābīl, kwa kuwa hakuwa mcha-Mungu. Qābīl alimhusudu ndugu yake na akasema, «Nitakuua.» Hābīl akajibu, «Kwa hakika Mwenyezi Mungu Huikubali sadaka itokayo kwa wale wenye kumuogopa.»
Al-Ma'idah 5:27
Inapakia kisomo…
0:00