وَأَوۡفُواْ بِعَهۡدِ ٱللَّهِ إِذَا عَٰهَدتُّمۡ وَلَا تَنقُضُواْ ٱلۡأَيۡمَٰنَ بَعۡدَ تَوۡكِيدِهَا وَقَدۡ جَعَلۡتُمُ ٱللَّهَ عَلَيۡكُمۡ كَفِيلًاۚ إِنَّ ٱللَّهَ يَعۡلَمُ مَا تَفۡعَلُونَ ٩١
An-Nahl 16:91
سورة النحل
Makka
Aya: 91/128
Ukurasa 277
-
Ali Muhsin Al - Swahili translation
Na timizeni ahadi ya Mwenyezi Mungu mnapo ahidi, wala msivunje viapo baada ya kuvithibitisha, ilihali mmekwisha mfanya Mwenyezi Mungu ndiye mdhamini wenu. Hakika Mwenyezi Mungu anayajua myatendayo. -
Abdullah Muhammad & Nassir Khamis
الترجمة السواحلية - عبد الله محمد وناصر خميس
Na jilazimisheni kutekeleza kila ahadi mliyojilazimisha nayo juu ya nafsi zenu, baina yenu nyinyi na Mwenyezi Mungu, Aliyetukuka, au baina yenu na watu katika yale yasiyoenda kinyume na Kitabu cha Mwenyezi Mungu na Sunnah ya Nabii Wake. Wala msirudi nyuma kwenye viapo mlivyovitilia mkazo, na hali mlimfanya Mwenyezi Mungu Ndiye mdhamini na msimamizi mlipomuahidi. Hakika Mwenyezi Mungu Anayajua mnayoyafanya na Atawalipa kwayo.
An-Nahl 16:91
Inapakia kisomo…
0:00