An-Nisa' 4:144

سورة النساء

Madina Aya: 144/176 Ukurasa 101

يَٰٓأَيُّهَا ٱلَّذِينَ ءَامَنُواْ لَا تَتَّخِذُواْ ٱلۡكَٰفِرِينَ أَوۡلِيَآءَ مِن دُونِ ٱلۡمُؤۡمِنِينَۚ أَتُرِيدُونَ أَن تَجۡعَلُواْ لِلَّهِ عَلَيۡكُمۡ سُلۡطَٰنࣰا مُّبِينًا ١٤٤

  1. Ali Muhsin Al - Swahili translation


    Enyi mlio amini! Msiwafanye makafiri kuwa ndio marafiki badala ya Waumini. Je, mnataka Mwenyezi Mungu awe na hoja iliyo wazi juu yenu?
  2. Abdullah Muhammad & Nassir Khamis

    الترجمة السواحلية - عبد الله محمد وناصر خميس

    Enyi mliomuamini Mwenyezi Mungu, Mtume Wake na mkafuata sheria Yake! Msiwapende na kuwategemea wenye kukanusha Dini ya Mwenyezi Mungu na mkaacha kuwapenda kuwategemea Waumini na kuwapenda. Je, mnataka kwa kuwapenda maadui wenu kumpa Mwenyezi Mungu, Aliyetukuka, hoja iliyo wazi kuwa nyinyi si wakweli katika Imani yenu?

Soma sura nzima Tafsiri ya Kiarabu