وَلَئِنۡ أَصَٰبَكُمۡ فَضۡلࣱ مِّنَ ٱللَّهِ لَيَقُولَنَّ كَأَن لَّمۡ تَكُنۢ بَيۡنَكُمۡ وَبَيۡنَهُۥ مَوَدَّةࣱ يَٰلَيۡتَنِي كُنتُ مَعَهُمۡ فَأَفُوزَ فَوۡزًا عَظِيمࣰا ٧٣
An-Nisa' 4:73
سورة النساء
Madina
Aya: 73/176
Ukurasa 89
-
Ali Muhsin Al - Swahili translation
Na ikikufikieni fadhila kutoka kwa Mwenyezi Mungu husema - kama kwamba hapakuwa mapenzi baina yenu naye: Laiti ningeli kuwa pamoja nao nikafanikiwa mafanikio makubwa. -
Abdullah Muhammad & Nassir Khamis
الترجمة السواحلية - عبد الله محمد وناصر خميس
Na itokeapo mkapata fadhila za Mola wenu na ngawira, wao wanasema, kwa uhasidi na majuto, kama kwamba hakukuwa na mapenzi ya waziwazi baina yenu, «Laiti mimi nilikuwa pamoja na wao nikafaulu kupata yale waliyoyapata: ya kuokoka, ushindi na ngawira.»
An-Nisa' 4:73
Inapakia kisomo…
0:00