إِنَّمَا كَانَ قَوۡلَ ٱلۡمُؤۡمِنِينَ إِذَا دُعُوٓاْ إِلَى ٱللَّهِ وَرَسُولِهِۦ لِيَحۡكُمَ بَيۡنَهُمۡ أَن يَقُولُواْ سَمِعۡنَا وَأَطَعۡنَاۚ وَأُوْلَٰٓئِكَ هُمُ ٱلۡمُفۡلِحُونَ ٥١
An-Nur 24:51
سورة النور
Madina
Aya: 51/64
Ukurasa 356
-
Ali Muhsin Al - Swahili translation
Haiwi kauli ya Waumini wanapo itwa kwa Mwenyezi Mungu na Mtume wake ili ahukumu baina yao, ila ni kusema: Tumesikia, na tumet'ii! Na hao ndio wenye kufanikiwa. -
Abdullah Muhammad & Nassir Khamis
الترجمة السواحلية - عبد الله محمد وناصر خميس
Ama Waumini wa kweli, msimamo wao ni kwamba wanapoitwa kwenda kuhukumiwa, katika ugomvi ulio kati yao, na Kitabu cha Mwenyezi Mungu na hukumu ya Mtume Wake, wanakubali uamuzi unaotolewa na wanasem, «Tumesikia tulioambiwa na tumemtii aliyetuita kwenye hilo.» Na hao ndio waliofaulu wenye kufuzu kupata matakwa yao kwenye mabustani ya Pepo yenye neema.
An-Nur 24:51
Inapakia kisomo…
0:00