وَٱلَّذِينَ ءَاتَيۡنَٰهُمُ ٱلۡكِتَٰبَ يَفۡرَحُونَ بِمَآ أُنزِلَ إِلَيۡكَۖ وَمِنَ ٱلۡأَحۡزَابِ مَن يُنكِرُ بَعۡضَهُۥۚ قُلۡ إِنَّمَآ أُمِرۡتُ أَنۡ أَعۡبُدَ ٱللَّهَ وَلَآ أُشۡرِكَ بِهِۦٓۚ إِلَيۡهِ أَدۡعُواْ وَإِلَيۡهِ مَـَٔابِ ٣٦
Ar-Ra'd 13:36
سورة الرعد
Madina
Aya: 36/43
Ukurasa 254
-
Ali Muhsin Al - Swahili translation
Na tulio wapa Kitabu wanafurahia uliyo teremshiwa. Na katika makundi mengine wapo wanao yakataa baadhi ya haya. Sema: Nimeamrishwa nimuabudu Mwenyezi Mungu, na wala nisimshirikishe. Kuendea kwake Yeye ndiyo ninaita, na kwake Yeye ndio marejeo yangu. -
Abdullah Muhammad & Nassir Khamis
الترجمة السواحلية - عبد الله محمد وناصر خميس
Na wale ambao tuliwapa Kitabu, miongoni mwa Mayahudi na Wanaswara, yoyote kati yao mwenye kukuamini, kama 'Abdullāh bin Salām na Najashi, wanaifurahia Qur’ani uliyoteremshiwa kwa kuwa inaenda sambamba na kile walichonacho. Na miongoni mwa wale wanaojiweka pamoja kukupinga, kama Sayyid na 'Aqib: maaskofu wawili wa Najran , na Ka'b bin al-Ashraf, wanaokanusha baadhi ya yale uliyoteremshiwa. Waambie, «Mwenyezi Mungu Ameniamrisha nimuabudu Yeye Peke Yake na nisimshirikishe chochote. Nawaita watu wamuabudu, na Kwake Peke Yake ndio marejeo yangu na marudio.
Ar-Ra'd 13:36
Inapakia kisomo…
0:00