وَإِذۡ قَالَ مُوسَىٰ لِقَوۡمِهِۦ يَٰقَوۡمِ لِمَ تُؤۡذُونَنِي وَقَد تَّعۡلَمُونَ أَنِّي رَسُولُ ٱللَّهِ إِلَيۡكُمۡۖ فَلَمَّا زَاغُوٓاْ أَزَاغَ ٱللَّهُ قُلُوبَهُمۡۚ وَٱللَّهُ لَا يَهۡدِي ٱلۡقَوۡمَ ٱلۡفَٰسِقِينَ ٥
As-Saff 61:5
سورة الصف
Madina
Aya: 5/14
Ukurasa 551
-
Ali Muhsin Al - Swahili translation
Na Musa alipo waambia watu wake: Enyi watu wangu! Kwa nini mnaniudhi, nanyi mnajua kuwa hakika mimi ni Mtume wa Mwenyezi Mungu niliye tumwa kwenu? Walipo potoka, Mwenyezi Mungu aliziachia nyoyo zao zipotoke. Na Mwenyezi Mungu hawaongoi watu wapotovu. -
Abdullah Muhammad & Nassir Khamis
الترجمة السواحلية - عبد الله محمد وناصر خميس
Wakumbushe watu wako, ewe Mtume, pindi aliposema Nabii wa Mwenyezi Mungu. Mūsā, amani imshukie, akiwaambia watu wake, «Kwa nini mnaniudhi kwa maneno na vitendo, na hali nyinyi mnajua kuwa mimi ni Mjumbe wa Mwenyezi Mungu kwenu?» Basi walipopotoka na kuwa kando na haki pamoja na kuwa wanaijua na wakaendelea juu ya hilo, Mwenyezi Mungu Aliziepusha nyoyo zao wasiukubali uongofu, ikiwa ni mateso kwao kwa sababu ya upotevu wao waliojichagulia wenyewe. Na Mwenyezi Mungu Hawaongozi watu wenye kutoka nje ya utiifu na njia ya haki.
As-Saff 61:5
Inapakia kisomo…
0:00