أَوَلَمۡ يَهۡدِ لَهُمۡ كَمۡ أَهۡلَكۡنَا مِن قَبۡلِهِم مِّنَ ٱلۡقُرُونِ يَمۡشُونَ فِي مَسَٰكِنِهِمۡۚ إِنَّ فِي ذَٰلِكَ لَأٓيَٰتٍۚ أَفَلَا يَسۡمَعُونَ ٢٦
AsSajdah 32:26
سورة السجدة
Makka
Aya: 26/30
Ukurasa 417
-
Ali Muhsin Al - Swahili translation
Je! Haijawabainikia kwamba kaumu ngapi tuliziangamiza kabla yao, nao wanapita katika maskani zao hizo? Hakika katika hayo zipo Ishara. Basi, je, hawasikii? -
Abdullah Muhammad & Nassir Khamis
الترجمة السواحلية - عبد الله محمد وناصر خميس
Kwani haikuwabainikia hawa wenye kumkanusha Mtume ni mara ngapi tuliwaangamiza ummah waliotangulia kabla yao na huku wanatembea kwenye makazi yao, wakawa wanayaona waziwazi, kama vile watu wa Hūd, Ṣāliḥ na Lūṭ? Hakika katika hayo kuna alama na mawaidha ya kutolea ushahidi ukweli wa Mitume waliowajia na urongo wa ushirikina walionao. Basi kwani hawasikii, hawa wenye kuwakanusha Mitume, mawaidha ya Mwenyezi Mungu na dalili Zake wakapata kunufaika nayo?
AsSajdah 32:26
Inapakia kisomo…
0:00