وَمَا كَانَ لَهُم مِّنۡ أَوۡلِيَآءَ يَنصُرُونَهُم مِّن دُونِ ٱللَّهِۗ وَمَن يُضۡلِلِ ٱللَّهُ فَمَا لَهُۥ مِن سَبِيلٍ ٤٦
Ash-Shura 42:46
سورة الشورى
Makka
Aya: 46/53
Ukurasa 488
-
Ali Muhsin Al - Swahili translation
Wala hawatakuwa na walinzi wa kuwanusuru mbele ya Mwenyezi Mungu. Na ambaye Mwenyezi Mungu amemwacha kupotea, hana njia yoyote. -
Abdullah Muhammad & Nassir Khamis
الترجمة السواحلية - عبد الله محمد وناصر خميس
Na hawa wenye kukanusha, Atakapowaadhibu Mwenyezi Mungu Siku ya Kiyama, hawatakuwa na wasaidizi na waokozi wenye kuwanusuru kutokana na adhabu ya Mwenyezi Mungu. Na yoyote yule ambaye Mwenyezi Mungu Amempoteza kwa sababu ya ukanushaji wake na udhalimu, hatakuwa na njia yenye kumfikisha kwenye haki hapa duniani, na kwenye Pepo kesho Akhera, kwa kuwa yeye atakuwa amezibiwa njia za kuokoka, kwani kuongoza na kupoteza viko mkononi mwa Mwenyezi Mungu, kutakasika na kutukuka ni Kwake, na haviko kwa mwingine.
Ash-Shura 42:46
Inapakia kisomo…
0:00