يُسَبِّحُ لِلَّهِ مَا فِي ٱلسَّمَٰوَٰتِ وَمَا فِي ٱلۡأَرۡضِۖ لَهُ ٱلۡمُلۡكُ وَلَهُ ٱلۡحَمۡدُۖ وَهُوَ عَلَىٰ كُلِّ شَيۡءࣲ قَدِيرٌ ١
At-Taghabun 64:1
سورة التغابن
Madina
Aya: 1/18
Ukurasa 556
-
Ali Muhsin Al - Swahili translation
Kinamtakasa Mwenyezi Mungu kila kilichomo katika mbingu na katika ardhi. Ufalme ni wake, na sifa njema ni zake. Na Yeye ni Mwenye uweza juu ya kila kitu. -
Abdullah Muhammad & Nassir Khamis
الترجمة السواحلية - عبد الله محمد وناصر خميس
Vinamtakasa Mwenyezi Mungu na sifa zisizonasibiana na Yeye vyote vilivyoko mbinguni na vilivyoko ardhini. Ni Wake Yeye Mwenyezi Mungu, kutakasika na kila upungufu ni Kwake, uendeshaji mambo usio na kizuizi katika kila kitu. Na Yeye Ndiye Mwenye sifa njema zilizo nzuri. Na Yeye juu ya kila kitu ni Muweza.
At-Taghabun 64:1
Inapakia kisomo…
0:00