يَٰٓأَيُّهَا ٱلَّذِينَ ءَامَنُوٓاْ إِنَّ مِنۡ أَزۡوَٰجِكُمۡ وَأَوۡلَٰدِكُمۡ عَدُوࣰّا لَّكُمۡ فَٱحۡذَرُوهُمۡۚ وَإِن تَعۡفُواْ وَتَصۡفَحُواْ وَتَغۡفِرُواْ فَإِنَّ ٱللَّهَ غَفُورࣱ رَّحِيمٌ ١٤
At-Taghabun 64:14
سورة التغابن
Madina
Aya: 14/18
Ukurasa 557
-
Ali Muhsin Al - Swahili translation
Enyi mlio amini! Hakika miongoni mwa wake zenu na watoto wenu wamo maadui zenu. Basi tahadharini nao. Na mkisamehe, na mkapuuza, na mkaghufiria basi hakika Mwenyezi Mungu ni Mwingi wa maghfira, Mwenye kurehemu. -
Abdullah Muhammad & Nassir Khamis
الترجمة السواحلية - عبد الله محمد وناصر خميس
Enyi mliomuamini Mwenyezi Mungu na Mtume Wake! Kwa kweli miongoni mwa wake zenu na wana wenu ni maadui wenu, wanawazuia nyinyi na njia ya Mwenyezi Mungu na wanawavunja moyo ya kumtii Mwenyezi Mungu, basi jihadharini nao wala msiwasikilize. Na iwapo mtayasamehe makosa yao, mkayapa mgongo na mkayaficha msiyatangaze, basi Mwenyezi Mungu ni Mwingi wa kusamehe ni Mwingi wa rehema, Atawasamehe nyinyi madhambi yenu, kwani Yeye, Aliyetakasika na kila upungufu, ni Mkubwa wa kusamehe ni Mkunjufu wa rehema.
At-Taghabun 64:14
Inapakia kisomo…
0:00