وَٱلَّٰٓـِٔي يَئِسۡنَ مِنَ ٱلۡمَحِيضِ مِن نِّسَآئِكُمۡ إِنِ ٱرۡتَبۡتُمۡ فَعِدَّتُهُنَّ ثَلَٰثَةُ أَشۡهُرࣲ وَٱلَّٰٓـِٔي لَمۡ يَحِضۡنَۚ وَأُوْلَٰتُ ٱلۡأَحۡمَالِ أَجَلُهُنَّ أَن يَضَعۡنَ حَمۡلَهُنَّۚ وَمَن يَتَّقِ ٱللَّهَ يَجۡعَل لَّهُۥ مِنۡ أَمۡرِهِۦ يُسۡرࣰا ٤
At-Talaq 65:4
سورة الطلاق
Madina
Aya: 4/12
Ukurasa 558
-
Ali Muhsin Al - Swahili translation
Na wale walio sita hedhi miongoni mwa wanawake wenu, ikiwa mnayo shaka, basi muda wa eda yao ni miezi mitatu, pamoja na ambao hawapati hedhi. Na wenye mimba eda yao mpaka watakapo zaa. Na anaye mcha Mwenyezi Mungu, Mwenyezi Mungu humfanyia mambo yake kuwa mepesi. -
Abdullah Muhammad & Nassir Khamis
الترجمة السواحلية - عبد الله محمد وناصر خميس
Na wanawake walioachwa ambao damu zao za hedhi zimekatika kwa utu uzima wao, mkitatizika mkawa hamjui: ni nini hukumu yao? Basi, eda lao ni miezi mitatu. Na wanawake wadogo ambao hawajaingia damuni, basi eda lao ni miezi mitatu vilevile. Na wanawake wajawazito, eda lao ni linamalizikia pale wanapozaa. Na yoyote atakayemuogopa mwenyezi Mungu na akatekeleza hukumu Zake, Atamfanyia mambo Yake yawe mepesi duniani na Akhera.
At-Talaq 65:4
Inapakia kisomo…
0:00