۞ قَٰلَ أَوَلَوۡ جِئۡتُكُم بِأَهۡدَىٰ مِمَّا وَجَدتُّمۡ عَلَيۡهِ ءَابَآءَكُمۡۖ قَالُوٓاْ إِنَّا بِمَآ أُرۡسِلۡتُم بِهِۦ كَٰفِرُونَ ٢٤
Az-Zukhruf 43:24
سورة الزخرف
Makka
Aya: 24/89
Ukurasa 491
-
Ali Muhsin Al - Swahili translation
Akasema (Mwonyaji): Hata nikikuleteeni yenye uwongofu bora kuliko mlio wakuta nao baba zenu? Wakasema: Sisi tunayakataa tu hayo mliyo tumwa. -
Abdullah Muhammad & Nassir Khamis
الترجمة السواحلية - عبد الله محمد وناصر خميس
Huyo Muonyaji, akiwa ni Mtume Muhammad, rehema ya Mwenyezi Mungu na amani zimshukie, na wale Mitume waliomtangulia, huwa akisema kuwaambia waliompinga wakitumia udanganyifu huu uliyotanguka, «Je, mtawafuata baba zenu , hata kama mimi nimewajia kutoka kwa Mola wenu na kitu chenye kuongoza zaidi kwenye njia ya haki na chenye kuonyesha zaidi njia ya uongofu kuliko kile mlichowakuta baba zenu wakikifuata cha dini na mila?” Na wao huwa wakisema kwa ushindani, ”Sisi ni wenye kuyapinga na kuyakanusha hayo mliyotumilizwa kwayo.”
Az-Zukhruf 43:24
Inapakia kisomo…
0:00