وَلَوۡ يُؤَاخِذُ ٱللَّهُ ٱلنَّاسَ بِمَا كَسَبُواْ مَا تَرَكَ عَلَىٰ ظَهۡرِهَا مِن دَآبَّةࣲ وَلَٰكِن يُؤَخِّرُهُمۡ إِلَىٰٓ أَجَلࣲ مُّسَمࣰّىۖ فَإِذَا جَآءَ أَجَلُهُمۡ فَإِنَّ ٱللَّهَ كَانَ بِعِبَادِهِۦ بَصِيرَۢا ٤٥
Fatir 35:45
سورة فاطر
Makka
Aya: 45/45
Ukurasa 440
-
Ali Muhsin Al - Swahili translation
Na lau kuwa Mwenyezi Mungu angeli wachukulia watu kwa waliyo yachuma, basi asingeli muacha juu ya ardhi hata mnyama mmoja. Lakini Yeye anawachukulia mpaka ufike muda maalumu. Basi ukifika muda wao basi hakika Mwenyezi Mungu ni Mwenye kuwaona waja wake baraabara. -
Abdullah Muhammad & Nassir Khamis
الترجمة السواحلية - عبد الله محمد وناصر خميس
Na lau Mwenyezi Mungu Angaliwatesa watu kwa madhambi na maasia waliyoyatenda, Hangaliacha juu ya mgongo wa ardhi mnyama yoyote anayetembea juu yake. Lakini Anawapa muhula na Anachelewesha kuwaadhibu mpaka wakati maalumu Aliyoupanga. Na wakati wa kuwaadhibu ukija , basi Mwenyezi Mungu kwa waja Wake ni Mjuzi, hakuna yoyote kati yao atakayefichika Kwake, na hakuna chochote miongoni mwa mambo yao kilicho mbali na ujuzi Wake, na Atawalipa wao kwa walichotenda, chema au kibaya.
Fatir 35:45
Inapakia kisomo…
0:00