مَّا يُقَالُ لَكَ إِلَّا مَا قَدۡ قِيلَ لِلرُّسُلِ مِن قَبۡلِكَۚ إِنَّ رَبَّكَ لَذُو مَغۡفِرَةࣲ وَذُو عِقَابٍ أَلِيمࣲ ٤٣
Fussilat 41:43
سورة فصلت
Makka
Aya: 43/54
Ukurasa 481
-
Ali Muhsin Al - Swahili translation
Huambiwi ila yale yale waliyo ambiwa Mitume wa kabla yako. Hakika Mola wako Mlezi bila ya shaka ni Mwenye maghfira, na ni Mwenye adhabu chungu. -
Abdullah Muhammad & Nassir Khamis
الترجمة السواحلية - عبد الله محمد وناصر خميس
Hawakwambii hao washirikina, ewe Mtume, isipokuwa kile ambacho washakisema kabla yao ummah waliopita kuwaambia Mitume wao. Basi vumilia juu ya kinachokupata katika njia ya ulinganizi kwa Mwenyezi Mungu. Hakika Mola wako ni Mwenye msamaha mwingi wa dhambi za wenye kutubia, ni mwenye mateso kwa mwenye kuendelea kumkufuru na kumkanusha.
Fussilat 41:43
Inapakia kisomo…
0:00