وَلَقَدۡ ءَاتَيۡنَا مُوسَى ٱلۡكِتَٰبَ فَٱخۡتُلِفَ فِيهِۚ وَلَوۡلَا كَلِمَةࣱ سَبَقَتۡ مِن رَّبِّكَ لَقُضِيَ بَيۡنَهُمۡۚ وَإِنَّهُمۡ لَفِي شَكࣲّ مِّنۡهُ مُرِيبࣲ ١١٠
Hood 11:110
سورة هود
Makka
Aya: 110/123
Ukurasa 234
-
Ali Muhsin Al - Swahili translation
Na kwa yakini tulimpa Musa Kitabu; zikazuka khitilafu ndani yake. Na lau kuwa si neno lilio kwisha tangulia kutoka kwa Mola wako Mlezi, bila ya shaka ingeli hukumiwa baina yao. Na hakika wao wamo katika shaka juu yake inayo wahangaisha. -
Abdullah Muhammad & Nassir Khamis
الترجمة السواحلية - عبد الله محمد وناصر خميس
Na hakika tulimpa Mūsā Kitabu , nacho ni Taurati, wakatafautiana watu wake juu yake: baadhi yao walikiamini na wengine walikikanusha, kama walivyofanya watu wako kuhusu Qur'ani. Na lao si neno lililotangulia kutoka kwa Mola wako la kutowaharakishia adhabu viumbe Wake, ingaliwashukia wao duniani kwao hukumu ya Mwenyezi Mungu ya kuwaangamiza wenye kukanusha na kuwaokoa Waumini. Na makafiri wa watu wako, miongoni mwa mayahudi na washirikina, ewe Mtume, wako kwenye shaka inayowatia wasiwasi juu hii Qur'ani.
Hood 11:110
Inapakia kisomo…
0:00