تِلۡكَ مِنۡ أَنۢبَآءِ ٱلۡغَيۡبِ نُوحِيهَآ إِلَيۡكَۖ مَا كُنتَ تَعۡلَمُهَآ أَنتَ وَلَا قَوۡمُكَ مِن قَبۡلِ هَٰذَاۖ فَٱصۡبِرۡۖ إِنَّ ٱلۡعَٰقِبَةَ لِلۡمُتَّقِينَ ٤٩
Hood 11:49
سورة هود
Makka
Aya: 49/123
Ukurasa 227
-
Ali Muhsin Al - Swahili translation
Hizi ni katika khabari za ghaibu tunazo kufunulia. Hukuwa ukizijua wewe, wala watu wako, kabla ya hii. Basi subiri! Hakika Mwisho ni wa wachamngu. -
Abdullah Muhammad & Nassir Khamis
الترجمة السواحلية - عبد الله محمد وناصر خميس
Habari hiyo tuliyokuhadithia kuhusu Nūḥ na watu wake ni miongoni mwa habari za ghaibu zilizopita, ambazo tunakuletea wahyi juu yake, hukuwa ukizijua, wewe wala watu wako, kabla ya maelezo haya. Basi subiri juu ya ukanushaji wa watu wako na makero yao wanayokufanyia kama walivyosubiri Manabii huko nyuma. Na mwisho mwema wa duniani na Akhera ni wa waogopao wanaomcha Mwenyezi Mungu.
Hood 11:49
Inapakia kisomo…
0:00