قَالُواْ يَٰشُعَيۡبُ أَصَلَوٰتُكَ تَأۡمُرُكَ أَن نَّتۡرُكَ مَا يَعۡبُدُ ءَابَآؤُنَآ أَوۡ أَن نَّفۡعَلَ فِيٓ أَمۡوَٰلِنَا مَا نَشَٰٓؤُاْۖ إِنَّكَ لَأَنتَ ٱلۡحَلِيمُ ٱلرَّشِيدُ ٨٧
Hood 11:87
سورة هود
Makka
Aya: 87/123
Ukurasa 231
-
Ali Muhsin Al - Swahili translation
Wakasema: Ewe Shua'ibu! Ni sala zako ndizo zinazo kuamrisha tuyaache waliyo kuwa wakiyaabudu baba zetu, au tuache kufanya tupendavyo katika mali zetu? Ama hakika wewe ni mstahamilivu kweli na mwongofu! -
Abdullah Muhammad & Nassir Khamis
الترجمة السواحلية - عبد الله محمد وناصر خميس
Wakasema, «Ewe Shu'ayb, je swala hii ambayo unaendelea nayo ndiyo inayokuamuru wewe kwamba sisi tuache masanamu na mizimu ambayo baba zetu wanaabudu, au kwamba sisi tujizuie tusitumie njia tuziwezazo za hila na vitimbi katika kuchuma mali yetu?» Wakasema kwa njia ya kumcheza shere, «Wewe ndiye mwenye akili na hodari wa mipango ya usimamizi wa mali.»
Hood 11:87
Inapakia kisomo…
0:00