أَلَمۡ تَرَ أَنَّ ٱلۡفُلۡكَ تَجۡرِي فِي ٱلۡبَحۡرِ بِنِعۡمَتِ ٱللَّهِ لِيُرِيَكُم مِّنۡ ءَايَٰتِهِۦٓۚ إِنَّ فِي ذَٰلِكَ لَأٓيَٰتࣲ لِّكُلِّ صَبَّارࣲ شَكُورࣲ ٣١
Luqman 31:31
سورة لقمان
Makka
Aya: 31/34
Ukurasa 414
-
Ali Muhsin Al - Swahili translation
Kwani huoni kwamba marikebu hupita baharini zikichukua neema za Mwenyezi Mungu, ili kukuonyesheni baadhi ya Ishara zake? Hakika katika haya zipo Ishara kwa kila mwenye kusubiri, mwenye kushukuru. -
Abdullah Muhammad & Nassir Khamis
الترجمة السواحلية - عبد الله محمد وناصر خميس
Kwani huoni, ewe mtazamaji, kwamba majahazi yanayotembea baharini kwa amri ya Mwenyezi Mungu ni neema itokayo Kwake kwa viumbe Wake, Apate kuwaonyesha utendakazi Wake na hoja Zake kwenu za kuwafanya nyinyi mzingatie? Hakika katika kupitisha majahazi baharini kuna dalili nyingi kwa kila mvumilivu sana wa kuyaepuka yaliyoharamishwa na Mwenyezi Mungu na katika kumtii Yeye na kuyavumilia mambo yaliyokadiriwa na Yeye, mwingi wa kushukuru neema Zake.
Luqman 31:31
Inapakia kisomo…
0:00