أَنِ ٱعۡمَلۡ سَٰبِغَٰتࣲ وَقَدِّرۡ فِي ٱلسَّرۡدِۖ وَٱعۡمَلُواْ صَٰلِحًاۖ إِنِّي بِمَا تَعۡمَلُونَ بَصِيرࣱ ١١
Saba' 34:11
سورة سبأ
Makka
Aya: 11/54
Ukurasa 429
-
Ali Muhsin Al - Swahili translation
(Tukamwambia:) Tengeneza nguo za chuma pana, na kadiria sawa katika kuunganisha. Na tendeni mema. Hakika Mimi nayaona vyema mnayo yatenda. -
Abdullah Muhammad & Nassir Khamis
الترجمة السواحلية - عبد الله محمد وناصر خميس
(Na tulikwambia, ewe Dāwūd,) «Tengeneze nguo za chuma zilizotimia na zilizo pana, na ukadirie vipimo vya misumari katika vikuku vya kuunganisha nguo hizo za chuma, na usikifanye kikuku kuwa kidogo kwani kitakuwa dhaifu, na kwa hivyo hizo nguo za chuma hazitaweza kumkinga (mwenye kuzivaa). Na usizifanye kubwa zikawa nzito kwa mwenye kuzivaa. Na ufanye, ewe Dāwūd, wewe na watu wako, vitendo vya kumtii Mwenyezi Mungu, kwani mimi kwa mnayoyafanya ni Mwenye kuyaona, hakifichamani kwangu kitu chochote katika hivyo.»
Saba' 34:11
Inapakia kisomo…
0:00