وَمَآ أَمۡوَٰلُكُمۡ وَلَآ أَوۡلَٰدُكُم بِٱلَّتِي تُقَرِّبُكُمۡ عِندَنَا زُلۡفَىٰٓ إِلَّا مَنۡ ءَامَنَ وَعَمِلَ صَٰلِحࣰا فَأُوْلَٰٓئِكَ لَهُمۡ جَزَآءُ ٱلضِّعۡفِ بِمَا عَمِلُواْ وَهُمۡ فِي ٱلۡغُرُفَٰتِ ءَامِنُونَ ٣٧
Saba' 34:37
سورة سبأ
Makka
Aya: 37/54
Ukurasa 432
-
Ali Muhsin Al - Swahili translation
Na si mali yenu wala watoto wenu watakao kukaribisheni kwetu muwe karibu, isipo kuwa aliye amini na akatenda mema. Hao basi watapata malipo mardufu kwa walio yafanya. Nao watakuwa salama katika maghorofa. -
Abdullah Muhammad & Nassir Khamis
الترجمة السواحلية - عبد الله محمد وناصر خميس
Hayakuwa mali yenu na watoto wenu ni vitu vya kuwafanya nyinyi muwe karibu na sisi, na daraja zenu ziwekwe juu, lakini wenye kumuamini Mwenyezi Mungu na wakafanya matendo mema, basi hao watapata malipo ya nyongeza: kwa jema moja kwa kumi mfano wake mpaka kiwango cha nyongeza Anachokitaka Mwenyezi Mungu. Na wao watakuwa kwenye Pepo ya juu kwa juu, wakiwa wamesalimika na adhabu, kifo na mambo ya huzuni.
Saba' 34:37
Inapakia kisomo…
0:00