وَمَا كَانَ هَٰذَا ٱلۡقُرۡءَانُ أَن يُفۡتَرَىٰ مِن دُونِ ٱللَّهِ وَلَٰكِن تَصۡدِيقَ ٱلَّذِي بَيۡنَ يَدَيۡهِ وَتَفۡصِيلَ ٱلۡكِتَٰبِ لَا رَيۡبَ فِيهِ مِن رَّبِّ ٱلۡعَٰلَمِينَ ٣٧
Yunus 10:37
سورة يونس
Makka
Aya: 37/109
Ukurasa 213
-
Ali Muhsin Al - Swahili translation
Na haiwezekani Qur'ani hii kuwa imetungwa na haitoki kwa Mwenyezi Mungu. Lakini hii inasadikisha yaliyo tangulia, na ni mfafanuo wa Kitabu kisicho na shaka ndani yake, kutokana na Mola Mlezi wa viumbe vyote. -
Abdullah Muhammad & Nassir Khamis
الترجمة السواحلية - عبد الله محمد وناصر خميس
Haikuwa ni yenye kumkinika kwa yoyote kuja nayo Qur’ani hii kutoka kwa asiyekuwa Mwenyezi Mungu, sababu ni kwamba hakuna yoyote awezae kufanya hilo miongoni mwa viumbe. Lakini Mwenyezi Mungu Aliiteremsha kusadikisha vitabu alivyowateremshia Manabii Wake, kwa kuwa dini ya Mwenyezi Mungu ni moja. Na katika hii Qur’ani kuna maelezo na ufafanuzi wa sheria ya Mwenyezi Mungu Aliyowaekea ummah wa Muhammad. Hapana shaka kwamba hii Qur’ani ni wahyi unaotoka kwa Mola wa viumbe wote.
Yunus 10:37
Inapakia kisomo…
0:00