ثُمَّ بَعَثۡنَا مِنۢ بَعۡدِهِم مُّوسَىٰ وَهَٰرُونَ إِلَىٰ فِرۡعَوۡنَ وَمَلَإِيْهِۦ بِـَٔايَٰتِنَا فَٱسۡتَكۡبَرُواْ وَكَانُواْ قَوۡمࣰا مُّجۡرِمِينَ ٧٥
Yunus 10:75
سورة يونس
Makka
Aya: 75/109
Ukurasa 217
-
Ali Muhsin Al - Swahili translation
Kisha baada yao tukamtuma Musa na Haruni kwa Firauni na waheshimiwa wake, kwa Ishara zetu. Wakajivuna, na wakawa watu wakosefu. -
Abdullah Muhammad & Nassir Khamis
الترجمة السواحلية - عبد الله محمد وناصر خميس
Kisha tukawatuma, baada Mitume hao, Mūsā na Hārūn, amani iwashukie, kwenda kwa Fir'awn na watukufu wa watu wake, wakiwa na miujiza yenye kuonesha dalili ya ukweli wao, wakafanya kiburi kwa kukataa kuikubali haki na wakawa ni watu washirikina, wahalifu na wakanushaji.
Yunus 10:75
Inapakia kisomo…
0:00