ذَٰلِكَ مِنۡ أَنۢبَآءِ ٱلۡغَيۡبِ نُوحِيهِ إِلَيۡكَۖ وَمَا كُنتَ لَدَيۡهِمۡ إِذۡ أَجۡمَعُوٓاْ أَمۡرَهُمۡ وَهُمۡ يَمۡكُرُونَ ١٠٢
Yusuf 12:102
سورة يوسف
Makka
Aya: 102/111
Ukurasa 247
-
Ali Muhsin Al - Swahili translation
Hizi ni katika khabari za ghaibu tulizo kufunulia. Na hukuwa pamoja nao walipo azimia shauri yao, walipo fanya njama zao wakizua vitimbi. -
Abdullah Muhammad & Nassir Khamis
الترجمة السواحلية - عبد الله محمد وناصر خميس
Hayo yaliyotajwa ya habari za Yūsuf ni miongoni mwa habari za ghaibu, tunakuelezea , ewe Mtume, kwa njia ya wahyi. Na hukuwako pamoja na ndugu zake Yūsuf walipompangia kumtia kisimani na wakamfanyia hila yeye na baba yake. Hii inaonesha dalili ya ukweli wako na kwamba Mwenyezi Mungu Anakuletea wahyi.
Yusuf 12:102
Inapakia kisomo…
0:00