قَالُواْ يَٰٓأَبَانَآ إِنَّا ذَهَبۡنَا نَسۡتَبِقُ وَتَرَكۡنَا يُوسُفَ عِندَ مَتَٰعِنَا فَأَكَلَهُ ٱلذِّئۡبُۖ وَمَآ أَنتَ بِمُؤۡمِنࣲ لَّنَا وَلَوۡ كُنَّا صَٰدِقِينَ ١٧
Yusuf 12:17
سورة يوسف
Makka
Aya: 17/111
Ukurasa 237
-
Ali Muhsin Al - Swahili translation
Wakasema: Ewe baba yetu! Hakika tulikwenda kushindana na tukamwacha Yusuf penye vitu vyetu. Basi mbwa mwitu akamla. Lakini wewe hutuamini ijapo kuwa tunasema kweli. -
Abdullah Muhammad & Nassir Khamis
الترجمة السواحلية - عبد الله محمد وناصر خميس
Wakasema, «Ewe baba yetu! Sisi tulikwenda tukawa tunashindana kukimbia na kurusha mishale, na tukamuacha Yūsuf kwenye vyombo vyetu na nguo zetu; na hatukufanya kasoro katika kumtunza, kwa kuwa tulimuacha mahali pa amani petu, na hatukumuacha isipokuwa kwa wakati mchache, mbwamwitu akamla. Na wewe hutatuamini, ingawa sisi ni wenye sifa ya ukweli, kwa sababu ya mapenzi yako makubwa kwa Yūsuf.
Yusuf 12:17
Inapakia kisomo…
0:00