يَـٰٓأَيُّهَا ٱلنَّبِيُّ إِذَا جَآءَكَ ٱلۡمُؤۡمِنَٰتُ يُبَايِعۡنَكَ عَلَىٰٓ أَن لَّا يُشۡرِكۡنَ بِٱللَّهِ شَيۡـٔٗا وَلَا يَسۡرِقۡنَ وَلَا يَزۡنِينَ وَلَا يَقۡتُلۡنَ أَوۡلَٰدَهُنَّ وَلَا يَأۡتِينَ بِبُهۡتَٰنٖ يَفۡتَرِينَهُۥ بَيۡنَ أَيۡدِيهِنَّ وَأَرۡجُلِهِنَّ وَلَا يَعۡصِينَكَ فِي مَعۡرُوفٖ فَبَايِعۡهُنَّ وَٱسۡتَغۡفِرۡ لَهُنَّ ٱللَّهَۚ إِنَّ ٱللَّهَ غَفُورٞ رَّحِيمٞ
Ewe Nabii! Watakapo kujia wanawake Waumini wanakuahidi ya kwamba hawatamshirikisha Mwenyezi Mungu na chochote, wala hawataiba, wala hawatazini, wala hawatawauwa watoto wao, wala hawataleta uzushi wanao uzua tu wenyewe baina ya mikono yao na miguu yao, wala hawatakuasi katika jambo jema, basi peana nao ahadi, na uwatakie maghfira kwa Mwenyezi Mungu. Hakika Mwenyezi Mungu ni Mwingi maghfira, Mwenye kurehemu.
Ali Muhsin Al - Swahili translation
Ewe Nabii! Wakiwajia nyinyi wanawake wenye kumuamini Mwenyezi Mungu na Mtume Wake na kuwaahidi kuwa hawatamshirikisha Mwenyezi Mungu katika kumuabudu, wala hawataiba chochote, wala hawatazini, wala hawataua watoto wao baada ya kuzaliwa au kabla yake, wala hawatawanasibishia waume zao watoto wasiotokana na wao, wala hawataenda kinyume na wewe katika jema unalowaamrisha kwalo, basi waahidi kwa hayo na uwaombee msamaha kutoka kwa Mwenyezi Mungu. Hakika Mwenyezi Mungu ni Mwenye kusamehe sana dhambi za waja Wake wenye kutubia na ni Mwenye kuwarehemu.
الترجمة السواحلية - عبد الله محمد وناصر خميس