هُوَ ٱلَّذِي بَعَثَ فِي ٱلۡأُمِّيِّـۧنَ رَسُولٗا مِّنۡهُمۡ يَتۡلُواْ عَلَيۡهِمۡ ءَايَٰتِهِۦ وَيُزَكِّيهِمۡ وَيُعَلِّمُهُمُ ٱلۡكِتَٰبَ وَٱلۡحِكۡمَةَ وَإِن كَانُواْ مِن قَبۡلُ لَفِي ضَلَٰلٖ مُّبِينٖ
Yeye ndiye aliye mpeleka Mtume kwenye watu wasio jua kusoma, awasomee Aya zake na awatakase, na awafunze Kitabu na hikima, ijapo kuwa kabla ya haya walikuwa katika upotofu ulio dhaahiri.
Ali Muhsin Al - Swahili translation
Mwenyezi Munu, kutakasika na kila upungufu ni Kwake, Ndiye Aliyetuma kwa Waarabu, wasiojua kusoma wala kuwa na kitabu wala kumbukumbu zozote za utume, Mtume anayetokamana na wao aliyetumwa kwa watu wote, awasomee Qur’ani na awatakase wao na itikadi mbovu na tabia mbaya, na awafundishe wao Qur’ani na Sunnah. Na wao, kwa kweli, tangu alipokuwa hajatumilizwa, walikuwa kwenye ukengeukaji ulio waziwazi kwa kuwa kando na haki. Na Mwenyezi Mungu, kutakasika na kila upungufu ni Kwake,
الترجمة السواحلية - عبد الله محمد وناصر خميس